Mwili wa Dk. Raymond Simion ukitolewa kwenye chumba cha kulala wageni na polisi.
MTU
mmoja aliyedaiwa kuwa ni daktari wa jijini Mwanza, Raymond Simion (36)
amekutwa amekufa ndani ya chumba kwenye nyumba ya kulala wageni ‘gesti’
ijulikanayo kwa jina la Nesta iliyopo Ubungo NHC wilayani Kinondoni
jijini Dar.Taarifa kutoka katika gesti hiyo zinasema marehemu
alijiorodhesha kwenye kitabu cha wageni kuwa ni daktari wa Hosptali ya
Nyamagana jijini Mwanza na alikuja Dar kikazi kwa muda wa wiki moja.
Mauti yalimkuta akiwa na siku mbili tu tangu alipowasili.
Mmoja wa
wahudumu wa gesti hiyo ambaye hakupenda jina lake litajwe gazetini
alisema kuwa, daktari huyo alifika katika gesti hiyo Jumapili ya Mei 4,
mwaka huu na kuchukua chumba namba 102.
Alisema Jumatatu ya Mei 5, marehemu aliomba abadilishiwe chumba, akapewa namba 105 ambamo mauti yalimkutia.
Uwazi
lilifanikiwa kufika katika eneo la tukio na kufanya mahojiano na
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Ubungo NHC, Amani Sizian ambaye
alisema taarifa ya kifo cha daktari huyo aliipokea saa 9: 03 alasiri ya
siku ya tukio ambapo mhudumu wa gesti hiyo ndiye aliyempigia simu
kumjulisha.
Kiongozi
huyo aliendelea kusema kuwa mhudumu huyo alimweleza kwamba marehemu
baada ya kuchukua chumba Jumapili alitoka na kurudi saa 3:00 usiku
ambapo alilala, lakini kesho yake hakuonekana kutoka.
“Mhudumu
aliniambia kuwa baada ya kutomwona asubuhi, hawakumfuatilia hadi
ilipofika saa 9:00 alasiri ambapo walikwenda kumchungulia chumbani kwake
na kumwona katika hali ya kutokuwa hai.
“Ilibidi niende. Nilipofika tukakuta mlango umefungwa kwa ndani.
Katika
kumchungulia tulimwona mtu huyo akiwa amekaa kitandani bila kujigeuza
jambo lililonifanya nipige simu polisi ambao walifika na kuvunja mlango
na kumkuta akiwa amefariki dunia,” alisema mwenyekiti huyo.
Aliongeza
kuwa, katika chumba hicho alichofia mteja huyo, kulikutwa mabomba
mawili ya sindano ambapo moja lilikwishatumika, pia kulikuwa na mifuko
miwili yenye nguo na begi moja.
Polisi
waliuchukua mwili na kuupeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili. Hata
hivyo, ndugu wa marehemu walipatikana na mwili kufanyiwa uchunguzi na
daktari kisha kuuchukua na kuusafirisha kwenda Mwanza kwa mazishi.
Kamanda
wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, ACP Camilius Wambura alithibitisha
kutokea kwa tukio hilo na kusema: “Marehemu alikutwa na mabomba mawili
ya sindano, moja lilishatumika na lilikuwa na masalia ya damu. Pia
kulikuwa na kete moja ya vitu vinavyodhaniwa kuwa ni madawa ya kulevya.
Post a Comment