POLISI TANZANIA WAHAKIKISHIA USALAMA WA RAIA DHIDI YA AL SHABAABU A+ A- Print Email PRINCE MEDIA TZ Link Author Title: POLISI TANZANIA WAHAKIKISHIA USALAMA WA RAIA DHIDI YA AL SHABAABU Author: PRINCE MEDIA TZ Rating 5 of 5 Des: Mkuu wa kitengo cha kudhibiti ugaidi nchini, Kamishna msaidizi wa Polisi, Mabula Goyai, amesema Tanzania imejipanga kiusalama kufuatia ... Mkuu wa kitengo cha kudhibiti ugaidi nchini, Kamishna msaidizi wa Polisi, Mabula Goyai, amesema Tanzania imejipanga kiusalama kufuatia vitisho vya ugaidi kutoka kwa kundi la Al Shabaab nchini Kenya. Goyai ametoa rai kwa wananchi kushirikiana na vyombo vya usalama, kwa taarifa au viashiria vyovyote vya kutaka kuharibu hali ya usalama nchini. Hata hivyo amesema kwa sasa wananchi hawana uelewa juu ya masuala ya ugaidi, hivyo amesema Jeshi hilo litaendelea kushirikiana na taasisi sisizo za kiserikali, ili kuweza kutoa elimu hiyo kwa wananchi kuhusiana na masuala hayo. Pamoja na mambo mengine amesema baadhi ya wananchi wamekuwa sehemu ya kuishi na watu hao kwani wamekuwa wakiishi katika maeneo yasiyorasmi, hivyo ameiomba jamii kushirikiana kikalimifu na Jeshi hilo ili kuchukua tahadhari kabla ya matukio hayo kutokea. Kumbukumbu zinaonyesha kuwa, baada ya mwaka jana, wanamgambo wa kundi la Al Shabaab, kufanya mashambulio katika jengo la biashara la Westgate mjini Nairobi na kuua watu zaidi ya (70) na kuacha mamia ya watu wengine wakiwa wamejeruhiwa kundi hilo limekuwa likitoa vitisho vya kuvamia nchi mbalimbali zilizopo ukanda wa Afrika Mashariki, ikiwemo Tanzania.
Post a Comment