Kamanda Mkumbo aliwataja marehemu ambao hadi sasa wametambuliwa kuwani Mohama Kidela(32) mkazi wa Bugarika Jijini Mwanza,AlexMasatu(42)mkazi wa Musoma,Wangwe Morice(30) Afisa Elimu MsaidiziHalmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Mahemba Chacha(42)mkazi waSerengeti mkoani Mara,Thomas Mwita(40)ambaye ni Mchungaji wa kanisa laSDA mjini Kahama mkoani Shinyanga.
Pia Kamanda Mkumbo amewaomba watu mbalimbali kufika katika hospitaliya Rufaa ya Bugando Jijini Mwanza ili kuweza kutambua miili ya nduguzao kwani hadi sasa maiti sita bado hazijatambuliwa.
Majeruhi 33 bado wanaendelea na matibabu katika hospitali ya BugandoJijini Mwanza na majeruhi 11 bado wanaendelea na matibabu katikahospitali ya wilaya ya Magu mkoani Mwanza.
Katika hatua nyingine jeshi la polisi mkoani humu linamshikiliammiliki wa basi hilo,Masalu Jackson mkazi wa Majengo mjini Bundamkoani Mara ambaye alikamatwa wilayani Busega mkoani humu kufuatiaushirikiano wa jeshi la polisi na wananchi huku wakiendelea kumtafutaaliyekuwa dereva wa Basi hilo ambaye jina lake halijapatikanaalitoroka mara baada ya ajali kutokea.
Basi la Luhuye Express lenye namba za usajiri T 410 AWQ liliacha njiana kugonga nyumba ya marehemu Mwalimu,Lazaro Mbofu na kuibomoa yote nakisha kupinduka na watu 10 kufa papo hapo
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.