PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: ARUSHA TOURISM FESTIVAL KUFANYIKA OCTOBER 14
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Ngoma za utamaduni katika tamasha la Arusha Tourism Festival zikiwaburudisha wageni mbalimbali     Aliyekuwa afisa Utalii Mkoa wa Arusha Flo...
Ngoma za utamaduni katika tamasha la Arusha Tourism Festival zikiwaburudisha wageni mbalimbali 

  



Aliyekuwa afisa Utalii Mkoa wa Arusha Flora Basil alipokuwa akizungmza katika kongamano la Arusha Tourism Festival 

Majuto Omary Mwenyekiti wa Taswa Fc ya jijini Dar es Salaam akizungumza katika tamasha la Arusha Tourism Festival 



  

Na: Mwandishi wetu, Arusha



Tamasha la nane la Utalii na wanahabari, Arusha tourism Festival  linatarajiwa kufanyika  Octoba12 hadi 14, 2023  jijini Arusha kwa kuwashirikisha wanahabari na wadau wa sekta ya Utalii na Uhifadhi nchini.


Tamasha hilo, linaandaliwa na Taasisi ya Arusha Media kwa kushirikiana na Taasisi ya wanahabari ya MAIPAC   na Chama cha waandishi wa habari za michezo (TASWA).


Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mratibu wa Tamasha hilo, Mussa Juma, alisema tamasha la mwaka huu,litakuwa na matukio matatu, maonesho ya bidhaa za Utalii, Kongamano  kuhusu sekta ya Utalii na Uhifadhi  na michezo.


“Tunatarajia  kushirikisha watu zaidi 700, wakiwepo wafanyabiashara wa sekta ya Utalii,   Wataalam  wa utalii na Uhifadhi na  waandishi wa habari kutoka mikoa 10 nchini ambayo imekuwa na changamoto ya  migogoro baina ya wanyamapori na binaadamu”alisema


Juma alisema Octobar 12-14 kutakuwa na Maonesho, Octoba 13 kongamano la wadau wa Utalii  na Octobar 14 kutakuwa na michezo ambayo itashirikisha timu za Wanahabari na wadau wa Utalii.


“Tumeanza maandalizi ya Tamasha hili na mwaka huu, limeboreshwa zaidi  tofauti na miaka ya nyuma na tunatarajhia kuwakutanisha wadau wa sekta ya Utalii na Uhifadhi  na wanahabari ili kuwajengewa uwezo masuala mbali mbali ya Utalii na uhifadhi”alisema


Juma alisema Katika Tamasha hilo, ambalo tangu mwaka 2015, limekuwa likifanyika  kauli mbiu  mwaka huu, kupunguza migogoro baina ya wanyamapori na wananchi lakini pia kutakuwa na mada ya kadhaa ikiwepo  Ulinzi wa maeneo ya mapito ya wanyamapori, kuzuia biashara haramu ya wanyamapori na nyamapori  na umuhimu wa vyombo vya habari kukuza sekta ya Utalii .


“Tamasha hili linatarajiwa   kusaidia kukuza sekta ya Utalii na Uhifadhi  lakini kujenga uelewa mzuri kwa wanahabari juu ya mafanikio na changamoto za sekta hii lakini pia kwa kuwa tutakuwa katika maadhimisho ya kumbukumbu tangu kifo cha baba wa Taifa Mwalimu Nyerere tamko lake juu ya uhifadhi na Wanyamapori  la mwaka 1961 linatajadiliwa ”alisema


Juma alisema  wataalikwa  watendaji wa Taasisi za Uhifadhi  na Utalii, Shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori(TAWA) Taasisi ya Utafiti wa wanyamapori(TAWIRI), Jumuiya za hifadhi za Wanyamapori(WMA) Wakala wa Misitu na Nyuki (TFS) na Wawekezaji katika sekta ya Utalii.


“Tutaendelea kutoa taarifa juu ya maandalizi ya tamasha hili la Utalii na tunaomba wadau mbali mbali kuendelea kujitokeza kuliwezesha na kushiriki”alisema



Awali Mratibu wa Arusha Media, Andrea Ngobole akizungumzia michezo itakayofanyika  Octobar 14, alisema kutakuwa na mchezo wa soka, mpira wa pete,kuvuta kamba, kukimbiza kuku na mbio za magunia.


“ Kama mnakumbuka  timu ya TASWA Dar es Salaam  ndio walikuwa mabingwa watetezi katika tamasha la saba katika soka na mpira wa pete tayari wamethibitisha kuja kutetea ubingwa wao “alisema


 Ngobole alisema zawadi za mwaka huu,zitatangazwa  hivi karibuni  sambamba na wadhamini wote ambao watakuwa wamejitokeza.

Timu ya michezo ya waandishi wa habari za michezo wa Dar es SalaamTaswa Fc  ambao ni mabingwa watetezi wa Tamasha lililopita wamethibitisha kushiriki tena katika tamasha hili mwaka huu


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top