PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MBUNGE WA UINGEREZA TRACEY CROUCH AFURAHIA MANDHARI YA MLIMA KILIMANJARO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
     Mbunge wa Bunge la Uingereza, Tracey Crouch wa tatu kutoka kushoto pamoja na wenzake nane wakiwa na Mkurugenzi wa Big Expedition and Sa...

   


Mbunge wa Bunge la Uingereza, Tracey Crouch wa tatu kutoka kushoto pamoja na wenzake nane wakiwa na Mkurugenzi wa Big Expedition and Safaris Angel Minja katika geti la Lemosho kabla ya kuanza kupanda  Mlima Kilimanjaro, ambao ni mrefu zaidi barani Afrika




Na: Andrea Ngobole, MAIPAC

maipacarusha20@gmail.com


 Mbunge  wa Bunge la Uingereza, Tracey  Crouch anaendelea kupanda Mlima Kilimanjaro na Leo amefika kituo cha Moyr Hut mita takriban 4600 kutoka usawa wa bahari.


 Crouch anapanda  Mlima Kilimanjaro, akiwa na wanawake wenzake wanane kupitia kampuni ya Big Expedition and Safaris ya jijini Arusha na tangu ameanza kupanda amekuwa na furaha kubwa kupanda Mlima huku akifurahia kukaribia kileleni mwa Mlima Kilimanjaro.


Mbunge huyo ambaye yupo katika kampeni  ya kuchangisha fedha kufanikisha matibabu ya  Saratani ya Matiti kwa wagonjwa na kesho anatarajiwa kufika kituo cha Baranko.

 


Crouch ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Michezo wa Uingereza kati ya mwaka 2017/18  anatarajiwa kushuka Mlimani Agosti 5 na kupokewa na wadau mbalimbali wa Utalii 


 kampuni ya kimataifa ya Utalii ya Uingereza ya Action Challenge  kwa kushirikiana na Big Expedition and Safaris ndio  wanampandisha kileleni Mbunge huyo na wenzake katika safari iliyopewa jina la Delux VIP ambapo wanaopanda mlima wanapewa huduma za viwango vya  juu zaidi (VIP service).


Mbunge huyo, ameanza Julai 29,2023 kupanda mlima huo mrefu barani Afrika, kupitia njia ya Lemosho .


 

Mkurugenzi wa kampuni ya Big Expedition and Safaris, Angel Minja akizungumza na MAIPAC media amesema ujio wa Mbunge huyo wa Uingereza ni kazi nzuri ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia filamu ya  The Royal Tour.


"Wageni kama Hawa kuwapata sio rahisi hivyo tunampongeza Sana Rais Samia kuendelea kutangaza Utalii wetu vizuri"amesema.



Minja pia ameipongeza Wizara ya Maliasili na Utalii, Waziri Mohamed Mchengerwa na Katibu Mkuu Dk Hassan Abbas na wasaidizi wao kwa kazi nzuri wanayofanya kuboresha Utalii.


"Waziri wetu anafanya kazi nzuri na sisi kama wamiliki wa kampuni za Utalii tunampongeza na tunamuunga mkono"amesema.


Minja amesema kampuni yao ambayo mwaka huu imetimiza miaka 20 tangu kuanzishwa imekuwa na mafanikio hasa kutokana na kuweza kupokea wageni wengi maarufu Duniani.


"Sisi pia tunajitahidi sana kutoa huduma bora zenye viwango vya kimataifa na nzuri kwa wageni ndio sababu wageni maarufu Duniani wanapitia kampuni yetu ambayo ni ya wazawa"amesema.


Amesema hivi karibuni walipokea wageni ambao ni mabalozi wa Utalii kutoka nchini Uingereza lakini pia familia za watoto wa viongozi wakubwa katika Mataifa yaliyoendelea wamekuwa wakitumia kampuni yao .

Mbunge wa Bunge la Uingereza, Tracey Crouch wa tatu kutoka kushoto na wenzake nane wakiwa na Mkurugenzi wa Big Expedition and Safaris Angel Minja katika geti la Lemosho kabla ya kuanzia kupanda  Mlima Kilimanjaro ambao ni mrefu zaidi barani Afrika




       

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top