Na: Mwandishi wetu, Meatu.
Taasisi ya Friedkin Conservation Fund (FCF) na Mwiba Holding Ltd zimetoa zaidi ya sh232milioni kugharamia Tembo kufungwa mikanda ya kusoma mawimbi (Collar) katika eneo la Ranchi ya wanyamapori ya Mwiba na Jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori ya Makao ili kudhibiti migogoro baina ya wananchi na Tembo
Mikanda ya imefungwa kwa Tembo viongozi wa makundi 10 na maafisa wa Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori nchini(TAWIRI),wakishirikiana na maafisa wa Mamlaka ya usimamizi wanyamapori nchini(TAWA).
Mikanda hiyo, inawezesha kuwafatilia Tembo kabla hawajafanya uharibifu wa kula mazao na kuhavamia makazi ya Wananchi katika eneo hilo lililopo wilaya ya Meatu.
Meneja miradi wa shirika la Friedkin Conservation Fund Tanzania, Aurelia Mtui, amesema mikanda hiyo,inalenga kuwafatilia Tembo katika eneo hilo na kupunguza migogoro za wananchi kwani tafiti za TAWIRI zinaeleza asilimia 99 ya migogoro ya wanyamapori na wananchi inatokana na Tembo.
Mtui amesema zoezi hilo limegharimu zaidi ya sh 232 milioni, ambazo ni fedha za kununua mikanda, kodi, gharama ya kusafirisha,gharama za wataalam na matumizi ya chopa na ndege katika kuwatafuta tembo wenye mikanda na kuwavalisha mikanda mipya.
"Tunaimani na kufungwa mikanda hiyo, itakuwa ni msaada mkubwa kwa jamii ambayo imekuwa ikilalamikia uvamizi wa tembo kila mara"amesema
Mkurugenzi Mkuu wa TAWIRI Dr.Ernest Mjingo ambaye ndiye anaongoza zoezi hilo amesema kufungwa kwa vifaa hivyo ni utekelezaji maagizo ya serikali kupunguza migogoro baina ya wanyamapori na wananchi.
Dr.Mjingo amesema mitambo hivyo, pia itasaidia kujua makundi ya tembo yalipo,jinsi wanavyotumia eneo lililohifadhiwa,umbali wanaotembea na kuwazuiwa kuingia katika maeneo ya wananchi kupitia uzio wa kielekroniki .
“Hili zoezi la endelevu, tulianza mwaka 2019 ambapo Tembo 18 viongozi wa makundi tuliwafunga hii mikandana ,sasa tembo 10 tunawafungua vifaa vya zamani na kuwafunga vifaa vipya kutokana na vilivyokuwepo kuanza kumaliza muda wake “alisema
Dr Mjingo amepongeza FCF na Mwiba holding Ltd kwa kuendelea kufadhili zoezi hilo ambalo ni muhimu katika uhifadhi.
Amesema technolojia iliyotumika kutengenezwa vifaa hivyo ni ya kwanza kutumika nchini kwa sababu inatumia umeme wa jua na hivyo kila Mkanda(collar) itakuwa na betri ambayo inatumia umeme wa jua.
Mratibu wa zoezi hilo Dr. Emmanuel Masenga amesema zoezi hilo lina umuhimu mkubwa katika shughuli za utafiti na uhifadhi.
"Tukiwafunga hii mikanda tunaweza kujua tabia na mienendo ya makundi ya tembo,wanapenda maeneo gani na ni kwanini lakini pia kujuwa mahusiano yao na wanyama wengine"amesema
Wakizungumzia zoezi hilo baadhi ya wakazi wa kijiji cha makao na Mwanuzi walipongeza kufungwa mkanda tembo.
"Imekuwa ni kawaida tembo kuvamia mashamba nakufika hadi mjini Mwanuzi na sasa watadhibitiwa"alisema Jeremiah Masanja.
Kampuni ya Mwiba Holding ltd imewekeza lanchi ya wanyamapori katika kijiji cha makao na kuwekeza shughuli nyingine za Utalii katik eneo la Makao WMA.
Post a Comment