Mchezo ukiendelea |
Msimamizi wa miradi ya chemchem association Nganashe Lukumay |
Mwenyekiti wa chemchem CUP, Erasto Belela |
Mwandishi wetu, MAIPAC
maipacarusha20@gmail.com
Babati.Taasisi ya chemchem association ambayo imewekeza katika shughuli za Utalii katika eneo la Jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori ya Burunge, imeanza kuwashirikisha wanawake katika uhifadhi kupitia mchezo wa soka.
Taasisi hiyo ambayo imekuwa ikiandaa ligi ya chemchem ya Soka timu za wanaume Killa mwaka yenye lengo la kupinga Vita ujangili, mwaka huu imeanza kwa kushirikisha timu za wanawake katika vijiji 10 ambavyo vinaunda Jumuiya hiyo.
Msimamizi wa miradi ya Jamii ya Taasisi hiyo, Nganashe Lukumay akizungumza katika Bonanza la timu za wanawake wa Kijiji Cha Mwada na Maweni amesema kuanzia mwaka huu wameanza kushirikisha timu za wanawake.
Nganashe anasema mwaka huu watakuwa na michezo ya Soka kwa wanawake ili kuwashirikisha katika kupiga Vita ujangili hasa wa Twiga katika eneo hilo.
Amesema taasisi hiyo pia itaendelea kuimarisha kuwajengea uwezo wa kujipatia vipato wanawake kupitia vikundi vyao lakini pia itaendelea kusaidia sekta nyingine kama elimu na afya.
Elizabeth Simba Mkufunzi wa vikundi vya ujasiriamali vya wanawake burunge WMA amesema chem chem association imekuwa na msaada mkubwa kwao kwani licha ya kuwapa fedha za miradi lakini inawashirikisha katika miradi na michezo.
"Hawa ni wawekezaji pekee mkoa wa Manyara ambao wanashirikisha Jamii nzima kupata miradi sisi wanawake tunapewa fedha miradi, tumepewa miradi ya ujasiriamali"amesema
Amesema hivi sasa wanashiriki katika uhifadhi wa wanyamapori kupitia michezo jambo ambalo litawaongezea uwezo kujua umuhimu wa uhifadhi.
Mwenyekiti wa Kamati ya michuano ya chemchem CUP, Erasto Belela amesema mwaka huu, michuano ya mwaka huu kutakuwa na ongezeko la timu na zawadi.
"Mwaka huu kauli mbiu yetu ni kuokoa Twiga na tunaimani mwaka huu kutakuwa na msisimko mkubwa"amesema.
TIMU za wanawake zinazoshiriki mashindano hayo |
Post a Comment