Afisa Wanyamapori Wilaya ya Meatu, Deusdedit Martin akizungumza na wadau wanavijiji |
Wawakilishi wa vijiji wilayani Meatu wakiwa katika kikao jumuiya ya hifadhi wanyamapori |
NA: MWANDISHI WETU
Vijiji 10 vinavyounda Jumuiya ya hifadhi ya wanyamapori ya Makao (Makao WMA), vinatarajia kupimwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi, ili kubainisha maeneo ya hifadhi na shughuli nyingine za kijamii.
Mpango huo wa matumizi bora ya ardhi, unatarajiwa kusaidia kupunguza migogoro baina ya shughuli za uhifadhi na shughuli nyingine katika eneo hilo ambalo linapakana na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Katibu wa Makao WMA, Jeremiah Bishoni alisema tayari mchakato umeanza kuvisaidia vijiji hivyo kupimwa ili kuwezesha kutenga maeneo mbali mbali kulingana na mahitaji.
"tunatarajia vijiji vikipimwa vyote, itasaidia kuwezesha mpango wa kupitia eneo zima la WMA na kufanikisha mpango wa usimamizi wa ardhi ya WMA( GNP) "alisema
Alisema Makao WMA katika kuboresha shughuli za uhifadhi na utalii inatarajiwa kuwa na vikao Februari 8 na wawekezaji katika eneo hilo na februari 9 wanatarajiwa kukutana na wajumbe wa baraza la WMA wa AA na mwekezaji katika eneo hilo.
Afisa Wanyamapori wilayani Meatu, Deusdedit Martin akizungumzia mikakati ya kuboresha shughuli za uhifadhi na Utalii, katika wilaya hiyo, alisema wamepanga kuvitembelea vijiji vyote vilivyopo ndani ya WMA na baadae kuwa na vikao na wadau wa uhifadhi na Utalii.
Akizungumzia changamoto ya ongezeko la Tembo kwenye makazi wa watu katika wilaya hiyo, alisema tayari halmashauri hiyo kwa kushirikiana na wadau wa uhifadhi kutoa elimu juu kuzuia Tembo kufika katika maeneo ya makazi ya watu.
"tuliwabaini kuna watu walikuwa wakiwafukuzia kwenye makazi ya watu Tembo ili kuzua tafrani "alisema.
Post a Comment