Mwenyekiti wa halamashauri wilaya ya Monduli Isack Copriano akizindua mradi wa uendeshaji na uzalishaji wa nyanda ya malisho wilaya ya Monduli unaotekelezwa na CORDS |
Katibu tawala wilaya ya Monduli akizungumza wakati wa Uzinduzi wa mradi huo |
Picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi wa mradi wa uendeshaji na uzalishaji wa nyanda za malisho |
Mmoja wa madiwani akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo |
Mwandishi wetu, MAIPAC
shirika la Maendeleo na Utafiti (CORDS) limezindua mradi wa uendeshaji na uzalishaji wa nyanda ya malisho wilaya ya Monduli mkoa wa Arusha,Ili kuwasaidia wafugaji kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi.
Katika wilaya hiyo, Wafugaji wamepata hasara ya shilingi 18.3 bilioni baada ya mifugo yao 127,786 kufa kwa Ukame katika msimu wa mwaka 2021/22.
Licha wa wafugaji kupata hasara hiyo,pia serikali imepoteza Kodi na tozo kiasi Cha shilingi 487.3 milioni ambazo zimekusanywa kama mifugo hiyo isingekufa.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Monduli, Isack Copriano akizindua mradi wa uendeshaji na uzalishaji wa nyanda ya malisho wilaya ya Monduli,Jana January 30,2023 amesema mradi huo utakuwa na manufaa makubwa katika wilaya hiyo
Mradi huo unaofadhiliwa na shirika la Maendeleo la umoja wa mataifa(UNDP ) kupitia program ya miradi midogo na mfuko wa Mazingira duniani (GEF) unatarajiwa kuwawezesha wafugaji kuwa na malisho ya uhakika.
Copriano alisema , Mifugo zaidi ya 127,786 katika wilaya hiyo imekufa kutokana na Ukame uliochangiwa na mabadiliko ya tabia nchi na hivyo mradi huo umekuja wakati muafaka kwani sasa wafugaji watapata elimu ya kuandaa nyanda za malisho na kupanda majani ya malisho katika maeneo yao.
"Tunashukuru sana Shirika la CORDS kuleta mradi huu kwani utakuwa na manufaa makubwa kwa wafugaji wa Monduli ambao wameathirika sana na mabadiliko ya tabia nchi na taarifa zinaeleza mwaka huu hali itakuwa mbaya zaidi"alisema
Kaimu Afisa mifugo wa wilaya Monduli,Yandu Marmo alisema kati ya vifo vya mifugo hiyo,127,786 ,Ng'ombe waliokufa ni 41,964, Mbuzi 31,213 na Kondoo 54,609.
"Hii hasara tulipiga kwa makisio ya chini mfano tuliweka kama Ng'ombe wangekuwa hai wangeuzwa kwa sh 300,000 kila mmoja hivyo hasara ni kubwa wamepata wafugaji"alisema
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkurugenzi wa shirika la CORDS Lilian Looloitai wanatarajia mradi huo kunufaisha zaidi 1476 kati yao wanawake 470 na wanaume na vijana 1006.
"Mradi huu tutautekeleza katika.vijiji vitatu ambavyo ni Emairele,Emurua na Eluai hapa Monduli"alisema
Akielezea mradi huo, Profesa Ismail Said Selemani alisema utakuwa na manufaa makubwa kwani kabla ya kupanda majani ya malisho katika maeneo hayo tafiti zimefanyika na kubaini aina ya majani ambayo yatastahimilo Ukame na udongo wa Monduli.
Profesa Selemani alisema lengo ya mradi huo ni kuboresha maisha ya wafugaji na endelezaji malisho bora na usimamizi wa nyanda za malisho.
sehemu ya washiriki wa uzinduzi wa mradi |
Akizungumzia mradi huo Mkurugenzi wa shirika Jumuiko la Maliasili Tanzania(TNRF) ambao ndio waratibu wa mradi huo aliwataka wafugaji kujifunza njia bora za ufugaji ikiwepo kuandaa malisho ya mifugo yao.
"Haya majani ambayo yatapandwa katika nyanda za malisho yanapatikana maeneo mbalimbali na ukipanda mara ya kwanza hautalazimika kupanda kila mwaka kama.mazao mengine"alisema
Wilaya ya Monduli Ina jumla ya Ng'ombe 234,876, Mbuzi 187,266 na Kondoo 162,185 na hivyo kuhitaji Ekali 1.218,267 za nyanda za malisho.
Mkurugenzi mtendaji wa TNRF Faustine Zacharia pamoja na afisa wa TNRF Doreen Tarimo wakifuatilia kwa makini uzinduzi wa mradi huo |
baadhi ya viongozi wa vijiji wakifuatilia uzinduzi wa mradi huo |
Post a Comment