PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: BENKI YA DUNIA WAAHIDI KUENDELEZA USHIRIKIANO NA TANZANIA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu Mwamba (kulia) akisalimiana na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia nc...

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu Mwamba (kulia) akisalimiana na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi 22 za Kundi Namba Moja Afrika, Dkt. Zarau Kibwe, aliyefika Ofisi za Hazina, Jijini Dodoma, kwa ajili ya kukutana na kufanya mazungumzo kuhusu ushirikiano wa Benki hiyo na Tanzania.

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu Mwamba, akiongoza mazungumzo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi 22 za Kundi Namba Moja Afrika, Dkt. Zarau Kibwe (wa tatu kushoto), aliyefika Ofisi za Hazina, Jijini Dodoma, kwa ajili ya kufahamiana na kufanya mazungumzo kuhusu ushirikiano kati ya Benki ya Dunia na Tanzania. Kulia ni Naibu Kamishna Idara ya Fedha za Nje Wizara ya Fedha na Mipango Bw. Robert Mtengule, kushoto ni Maafisa wa Wizara Idara ya Fedha za NJe Bw. Peter Masolwa na Bw. Charles Longo

Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu Mwamba (kulia) akisisitiza Jambo alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi 22 za Kundi Namba Moja Afrika, Dkt. Zarau Kibwe, aliyefika Ofisi za Hazina, Jijini Dodoma, kwa ajili ya kufahamiana na kufanya mazungumzo kuhusu ushirikiano wa Benki ya Dunia na Tanzania.

Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi 22 za Kundi Namba Moja Afrika, Dkt. Zarau Kibwe, akizungumza jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu Mwamba (kulia), Ofisi za Hazina, Jijini Dodoma, kwa ajili ya kufahamiana na kufanya mazungumzo kuhusu ushirikiano wa Benki ya Dunia na Tanzania.



 Na Benny Mwaipaja, Dodoma


KATIBU Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu Mwamba, amesema kuwa Serikali itaendelea kuimarisha uhusiano na ushirikiano wake na Benki ya Dunia ili kuharakisha maendeleo ya nchi kiuchumi na kijamii.


Dkt. Mwamba amesema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia anayesimamia, Kundi Namba Moja Afrika, Dkt. Zarau Kibwe, aliyefika Ofisi za Hazina, Jijini Dodoma, kujitambulisha.


Alisema kuwa mazungumzo yao yalilenga kuchambua fursa zinazopatikana kwenye Benki ya Dunia ambazo Tanzania kama Mwanahisa inaweza kuzifikia na kuzitumia kwa ajili ya maendeleo ya nchi na watu wake.


Kwa upande wake, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Dunia, anayesimamia maslahi ya nchi 22 za Kanda Namba Moja Afrika kwenye Taasisi hiyo kubwa ya Fedha Duniani, Dkt. Zarau Kibwe, alisema kuwa majadiliano yao yamekuwa na mafanikio makubwa.


Hii ni mara ya kwanza kwa Viongozi hao kukutana kikazi baada ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Dkt. Natu Mwamba kuteuliwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kushika wadhifa wa Katibu Mkuu na Mlipaji Mkuu wa Serikali, hivi karibuni.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top