Meneja miradi wa MAIPAC Deborah Makando akifafanua jambo kwa mtendaji mkuu wa Freedom house |
Mtendaji mkuu wa Freedom House wakili Daniel Lema akizungumza na Meneja utawala Andrea Ngobole ofisini kwake alipofanya ziara ya kikazi ofisini hapo |
Mtendaji Mkuu wa Freedom House, Wakili Daniel Lema akisistiza jambo kwa watendaji wa MAIPAC alipotembelea ofisi hizo |
Mtendaji mkuu wa freedom House Wakili Daniel Lema akipewa maelezo ya utendaji kazi wa MAIPAC na Meneja Utawala Andrea Ngobole. |
Mwandishi wetu, ARUSHA
Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Freedom House nchini Tanzania Wakili Daniel Naftali Lema amefurahishwa na Utendaji kazi wa Taasisi ya wanahabari ya kusaidia jamii za pembezoni (MAIPAC ).
Akizungumza katika Ofisi za MAIPAC baada ya kukutana na watendaji wa Taasisi hiyo na kupokea taarifa ya utekelezaji miradi mbalimbali, Lema amesema ameridhishwa na Utendaji kazi wa MAIPAC.
Amesema amefurahishwa baada ya kugundua taasisi hii yenye wanachama kutoka mikoa mbalimbali nchini wamejikita zaidi katika kusaidia kupaza sauti za jamii hizo za pembezoni na makundi maalum Ili kukabiliana na changamto za ardhi, haki za wanawake, watoto na walemavu .
“Ninawapongeza sana MAIPAC kwa kazi nzuri mnayoifanya ya kuandika habari za uchunguzi zinazosaidia jamii za pembezoni kujua haki zao na changamoto zinazowakabili ili iweze kupatiwa msaada na serikali na taasisi za kitaifa na kimataifa” amesema Na kuongeza
“Nimependa mpango mkakati wenu mnaoutekeleza sasa wa miaka mitatu na tutangalia objective ipi tutakayoona inafaa kupewa sapoti na freedom house ili muweze kuitimiza vema kazi zenu” amesema
Awali akimkaribisha ofisini hapo na kumtambulisha kwa baadhi ya wafanyakazi waliokuwepo ofisin hapo, Afisa utawala wa taasisi hiyo Andrea Ngobole amemwelezea mtendaju mkuu huyo kuwa taasisi ya MAIPAC ina wanachama 60 nchi nzima, ambao Huandika na kuchambua habari za jamii za pembezoni ili ziweze kusikika na kupatiwa suluhisho la kudumu na wenye mamlaka.
Amemshukuru kwa kutembelea ofisi hiyo na kuwa na dhamira ya dhati ya kujenga mahusiano mazuri kati ya maipac na freedom house katika kutekeleza na kuboresha baadhi ya maeneo yenye uhitaji wa haraka kama uandishi bora wa mpango mkakati na usimamizi wa miradi.
Naye Meneja miradi wa MAIPAC Deborah Makando amemuelezea kuwa taasisi imekuwa na maono mapana ya kutatua changamoto nyingi zinazokabali wanawake wa jamii za kifugaji kuwezesha kuwa na kipato endelevu, pia kuondokana na tatizo la ndoa za utotoni zinazowanyima haki ya kupata elimu na kuleta umaskini kwa jamii hizo.
Amesema kwa Sasa MAIPAC inatekeleza miradi wa uhifadhi wazingira,vyanzo vya maji na misitu kwa maarifa ya asili mradi ambao unaofadhiliwa na shirika la maendeleo la umoja wa mataifa (UNDP) kupitia program ya miradi midogo na mfuko wa Mazingira duniani (GEF).
Amesema mradi huo ambao unatekelezwa kwa wilaya tatu za Monduli, Longido na Ngorongoro unaratibiwa na jumuiko la maliasili Tanzania (TNRF) na unashirikisha halmashauri za wilaya hizo na wadau wengine.
viongozi wa maipac wakiagana na wakili Daniel Lema |
Mtendaji mkuu wa Freedom House akichukua maelezo toka kwa Meneja utawala Maipac |
Post a Comment