PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: SHIMIWI Yafanya Mapitio ya Katiba yake Kuboresha Utendaji Kazi
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
    Na Mwandishi Wetu, Dodoma   Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) limefanya Mkutano Mkuu Maalum na kufanya mapi...



 


 

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

 

Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) limefanya Mkutano Mkuu Maalum na kufanya mapitio ya Katiba yake pamoja na tathimini ya mashindano ya Shirikisho hilo yaliyofanyika jijini Tanga ili kuboresha utendaji kazi na kuleta tija kwa wa watumishi katika kuwahudumia wananchi.

 

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Shirikisho la Michezo ya Wizara na Idara za Serikali (SHIMIWI) Bw. Daniel Mwalusamba wakati akiongea na waandishi wa habari mwishoni mwa wiki mara baada ya mkutano huo jijini Dodoma.

 

“Kwa kuwa tulikuwa na michezo yetu ya SHIMIWI mwaka jana kule Tanga, tumetumia mkutano huu kufanya tathmini ya michezo hiyo, lengo likiwa ni kuhakikisha tunafanya tathimini na kubainisha upungufu yaliyojitokeza ili kupata ufumbuzi wa changamoto hizo na kuleta ufanisi zaidi katika Shirikisho" amesema Bw. Mwalusamba.

 

Bw. Mwalusamba amesema kuwa katika mkutano huo wajumbe wamejadili mambo mbalimbali kwa kuzingatia Katiba ambayo ndiyo mwongozo Mama wa Shirikisho hilo.

 

"Kwa msingi huo, tumejadili na kuazimia kukamilisha jambo mahususi la kukamilisha Katiba yetu ya Shirikisho, suala hili linahusu nani hasa ni wanachama wanaopaswa kushiriki katika michezo ya SHIMIWI”, amesema Bw. Mwalusamba.

 

Kwa msingi huo, wanaopaswa kushiriki katika michezo hiyo ni watumishi wote wa umma kutoka klabu za michezo katika Wizara, Idara, Mikoa na Wakala ambazo wafanyakazi wao ni Watumishi wa Serikali Kuu walio katika utumishi kwa mujibu wa Sheria Na. 8 ya mwaka 2002 inayohusu Utumishi wa Umma na Watumishi wa wakala wa Serikali kwa  Sheria Na. 30 ya mwaka 1997.

 

Katika kuimarisha utendaji na ufanisi wa michezo ya shirikisho hilo, Bw. Mwalusamba amebainisha changamoto ambazo wamezifanyia kazi kuwa ni pamoja na uratibu wa michezo ya SHIMIWI ikiwemo timu kuthibitisha kushiriki michezo hiyo na kufika kituo cha mashindano kwa wakati ili kuandaa na kupanga ratiba ya mashindano isiyo na migongano wakati wote wa mashindano.

 

Aidha, amewataka viongozi wa vilabu kufanya maandalizi ya timu zao mapema na kuwahusisha waajiri ili wajue na kalenda nzima ya Shirikisho hilo hatua itakayowawezesha waajiri kufanya maandalizi kuwezesha watumishi wa umma kushiriki kwenye mazoezi na kushiriki katika michezo ya SHIMIWI inayofanyika kila.

 

Kwa upande wake mshiriki wa mkutano huo Niwaheri Mburi ambaye ni Katibu wa Klabu ya Afya Sports kutoka Wizara ya Afya amewaomba wanamichezo kufanya mazoezi mapema ili wawe timamu kwa mashindano hayo na kutoa rai kwa waajiri kulipa kipaumbele suala la michezo ili kuimarisha afya za watumishi na kuleta tija katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku.  

 

Mkutano huo umefanyika kwa siku mbili ambapo ulitanguliwa na semina kwa viongozi hao kujua taratibu za kusajili vilabu vyao Baraza la Michezo la Taifa (BMT) ili wawe wanachama halali wa Shirikisho la SHIMIWI.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top