Waandishi wa habari nchini wametakiwa kuandika habari zenye manufaa Kwa jamii Kwa kuandika habari bunifu zinazolenga kuwakwamua wananchi kuondokana janga la umaskini.
Sekta ya habari na utangazaji ikitumika ipasavyo hususani vyombo vya habari mtandaoni kwa kuzingatia ukuaji wa teknolojia vinaharakisha zoezi la kuipasha jamii habari kwa wepesi na haraka zaidi hivyo kuwa chachu ya mabadiliko
Mkurugenzi wa taasisi ya wanahabari ya MAIPAC Bw Musa Juma akitoa hotuba katika mahafali ya 16 ya chuo cha uandishi wa habari Fanikiwa. PICHA na Marystela Bryson. |
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya wanahabari inayosaidia jamii za pembezoni nchini MAIPAC, Bw Musa Juma wakati akihutubia wahitimu na wazazi katika mahafali ya 16 ya Chuo cha Uandishi wa Habari na Utangazaji Fanikiwa Arusha yaliyofanyika katika ukumbi wa PPS jijini Arusha mapema leo.
Mkurugenzi huyo amesema kuwa ulimwengu wa sasa umekuwa, haswa katika eneo la sayansi na teknolojia hvyo wana habari wanapaswa kukimbia na ukuaji huo wa teknolojia kwa kuandika habari Bora na bunifu pia kuanzisha vyombo vya habari vya mitandaoni ambavyo vitawasaidia wao kujiajiri.
Wahitimu Wa Chuo Cha Uandishi wa Habari na Utangazazji Fanikiwa Ausha. PICHA na Marystela Bryson |
Musa Juma ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi MISA - TAN na Mkuu wa magazeti ya mwananchii Mkoani Arusha amewataka wahitimu hao wa ngazi ya Stashahada kuzingatia maadili wawapo kazini lakini pia kuwa wabunifu katika kuandika habari za mazingira, kilimo, uchumi, na mabadiliko ya TABIA NCHI ili kusaidia kuwaweka katika mazingira mazuri zaidi ya kihabari.
Naye mkuu wa chuo hicho Bwana Andrea Ngobole, amewataka wazazi wa wahitimu hao kuwaendeleza zaidi vijana hao katika chuo kikuu ili waendelee kupata elimu zaidi juu ya tasnia ya habari na sekta nyinginezo.
Mkuu wa Chuo cha uandishi wa habari na Utangazaji Fanikiwa Bw Andrea Ngobole akitoa hotuba kwa wahitimu wa chuo hicho mapema leo. PICHA NA Marystela Bryson. |
Aidha katika Mahafali Hayo wahitimu wapatao 40 wamehitimu mafunzo yao ya umahiri katika Tasnia ya habari na utangazaji ambapo pia wamedhamiria kwenda kuleta mabadiliko makubwa katika sekta ya habari na utangazaji.
Wahitimu wakiwa katika picha ya pamoja wakisikiliza Kwa makini hotuba ya mhgeni rasmi. |
Post a Comment