PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MILIONI MIA NNE ZA BODABODA ARUSHA ZAKWAPULIWA, WAMUOMBA RAIS SAMIA AWANUSURU.
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Jengo la Ofisi ya Umoja wa bodaboda wilaya ya ARUSHA Baadhi ya wajumbe wa bodaboda kutoka Kila Kata Jijini Arusha wakimsikiliza katibu wao...

 

Jengo la Ofisi ya Umoja wa bodaboda wilaya ya ARUSHA

Baadhi ya wajumbe wa bodaboda kutoka Kila Kata Jijini Arusha wakimsikiliza katibu wao alipokuwa akizungumza na wanahabari

Katibu wa umoja wa bodaboda Jijini Arusha akizungumza na wanahabari mapema Leo.


Katibu wa umoja wa bodaboda Jijini Arusha Hakimu Msemo akizungumza na wanahabari ofisini kwake mapema Leo.


NA: Mwandishi wetu, ARUSHA


Viongozi na wananachama wa chama cha waendesha bodaboda mkoa wa Arusha UBOJA wamemuomba Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassan kuingilia Kati ili waweze kupata fedha zao zaidi ya shilingi milioni 400 zilizotolewa kwenye akaunti ya chama katika mazingira ya Kutatanisha.

Akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake mapema leo katibu wa Umoja wa Bodaboda Jiji la Arusha Hakimu Msemo amesema kuwa fedha hizo zilikuwa ni msaada kutoka kwa wahisani pamoja na michango ya marejesho ya wanachama wa chama hicho


Amesema kuwa fedha hizo zimetolewa kwenye akaunt ya chama hicho kuanzia mwaka 2020 Kwa nyakati tofauti bila utaratibu na hivyo amemuomba Rais Samia kuwasaidia kupata haki yao.


Amesema pesa hizo zikirudishwa katika akaunti yao zitawasaidia kuendelea kukopeshana pikipiki Kwa wanachama wao zaidi ya elfu kumi na mbili waliopo katika Kata 25 za Jiji la Arusha.

Mwenyekiti wa umoja wa bodaboda Jijini Arusha Okero Constantine akizungumza na wanahabari


Kwa upande wake mwenyekiti umoja wa bodaboda jiji la Arusha Okelo Constantine amesema umoja huo una wanachama wasiopungua elfu kumi na mbili hivyo amemuomba Rais kutoa maelekezo kwa vyombo vya dola kulishughulikia suala Hilo kwa uharaka zaidi ili kuwakwamua wanachama wao wanaosubiri mgao wa pikipiki.



Amesema wanachama hao 12,000 huchangia mapato ya serikali Kwa kukata leseni ya udereva 70,000 Kila mmoja Kwa miaka mitano, Latra 17,000 Kila mwaka na mafuta ya elfu tano Kwa siku huwawezesha kuchangia mapato mengi Kwa Taifa.

Msemaji wa chama hicho Joshua Samwel amesema kuwa wapo wadau wanaotaka kuwasaidia bodaboda mia Moja Kwa kuanzia kulipa milioni mia Moja lakini wanakosa fedha za kuanzia Kwani akaunti yao Ina milioni mbili tu.

Mjumbe wa umoja huo Tumaini kivuyo amesema kuwa mwanzo wa maovu mengi huanzia kwenye umaskini wa vijana na hivyo kama watawezeshwa pesa hizo kurudi katika akaunti na kununua bodaboda na kugawa Kwa vijana Kila Kata.



About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top