PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MKUU WA MKOA MANYARA AZINDUA LIGI CHEMCHEM BABATI ILIYOGHARIMU SHILINGI MILION 35
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
Mgeni rasmi na baadhi ya viongozi wakikagua timu Baadhi ya mashabiki wakifuatilia mchezo wa ufunguzi wa ligu hiyo Mashabiki m...
Mgeni rasmi na baadhi ya viongozi wakikagua timu

Baadhi ya mashabiki wakifuatilia mchezo wa ufunguzi wa ligu hiyo


Mashabiki mbalimbali waliojitokeza kushuhudia ligi hiyo

akina mama wa upendo group wakitoa burudani

Kikundi cha akina mama wa kibarbaigi wakitoa burudani katika mashindano hayo
 

 Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Elexander Mnyeti juzi, amezindua ligi ya Chemchem ,inayoshirikisha timu 20, yenye lengo la kupiga vita ujangili ambayo itagharimu zaidi ya sh 35 milioni.

Akizungumza katika uzinduzi huo katika viwanja vya mdori, wilayani Babati, Mnyeti ambaye aliwakilishwa na Kamanda wa polisi mkoa wa Manyara, Augustine Senga alitaka timu zitakazoshiriki kucheza kwa nidhamu ili kufikia malengo ya ligi hiyo.

Mnyeti alisema,ligi hiyo pia inapaswa kutumika katika kuibua vipaji kwa wachezaji chipukizi ili kuweza kusajiliwa katika timu za ligi kuu.

"najua hapa kuna vipaji hivyo michezo hii ni fursa ya kujulikana zaidi na hivyo kuwa sehemu ya kutoa ajira kwa vijana  na kujenga afya"alisema

Katibu wa mashindano hayo,John Bura alisema jumla ya timu 20 za soka zinatarajia kushiriki michuano hiyo na kutakuwa na zawadi kwa mshindi wa kwanza hadi wa nne.

"pia kutakuwa na ligi ya wanawake ambayo itashirikisha timu tatu na washindi watapewa zawadi"alisema

Alisema katika michuano hiyo, mchezaji bora,mfungaji bora na timu yenye nidhamu, watapata zawadi na hivyo, akawataka kucheza soka la kuvutia.

Awali Meneja wa Chemchem ambao ni wadhamini wa ligi hiyo, Kanali mstaafu,Leonard Werema alisema, taasisi hiyo,  inayofanya shughuli za Utalii katika eneo hilo la hifadhi ya jamii ya Wanyamapori(WMA) ya  burunge, inataka ligi hiyo, kusaidia kutoa elimu ya kupiga vita ujangili na uhifadhi.

Werema alisema Chemchem imegharamia zaidi ya sh 35 milioni katika michuano hiyo, ikiwepo kuandaa uwanja na majengo kadhaa,zawadi, imetoa vifaa vya michezo kwa timu zote 23 na gharama nyingi za waamuzi na waratibu wa michuano hiyo chama cha soka wilaya ya Babati.

Katika mchezo wa ufunguzi, mabingwa watetezi, Mdori FC walipata ushindi wa magori 3-2 dhidi ya timu ya City Boys katika mchezo mkali uliochezwa kiwanja cha mdori.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top