Watuhumiwa
manne wa ujangili wamekamatwa na bunduki aina ya gobole na mtambo wa
kutengeneza silaha hizowilayani uvinza mkoani Kigoma.
Akizungumza
na waandishi wa habari meneja wa taasisi ya uhifadhi ya Friedkin
Conservation Fundi (FCF) Uvinza,mkoani Kigoma Audax Karurama alisema kukamatwa
watuhumiwa hao wa ujangili ni matokeo ya kazi ya intelijensia baina ya
askari Friedkin Conservation Fund ambao wanamiliki kitalu katika eneo
hilo na askari ya wanyamapori.
Karurama
alisema, katika maeneo ya Uvinza Msebehi kwa ushirikiano na askari wa
Wanyamapori eneo la kifura walifanikiwa kukamata mtuhumiwa wa ujangili
j akiwa na silaha aina ya gobore na Fundi wa kutengeneza
magobore. .
Alimtaja mtuhumiwa Huyo ambaye tayari anashikiliwa na jeshi la polisi kuwa ni Majaliwa Ramadhan(59) Mkazi wa kibaoni uvinza.
"Huyu mtuhumiwa tumemkuta pia na Goroli 20 Baruti 1/4 kilo, Mitego miwili ya waya na nyuzi za katani" alisema
Alisema katika msako huo wamefanikiwa kumkamata fundi wa magobole ,Laurent Sungura(55) akiwa na mtambo wake maeneo mlubanga -basanza .
Katika
msako huo eneo la Uvinza walikamata watuhumiwa wawili Wino Emily na
Zakia sinzi wote wa kijiji cha mvinza wakiwa na gobole.
"Tumewafuatilia
sana kwa ujanja wao wakaenda kusalimisha gobore kwa mwenyekiti wa
kijiji chao wakabaki na Smg Kwa hiyo bado Tunawafuatilia kwa karibu
ili kukamata hiyo silaha yao" alisema.
Post a Comment