Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimuonesha Mkuu wa Mkoa
wa Mara, Adam Malima mtego wa misumari uliotegwa na watu wasiojulikana
kwa lengo la kuzuia msafara wake wakati wa ziara yake ya kutatua mgogoro
wa mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani katika
wilaya ya Tarime mkoani Mara jana.
Tarime - Mara
.............................. .........................
WAZIRI
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameliagiza Jeshi la
Polisi wilaya ya Tarime mkoani Mara kumkamata na kumfungulia mashtaka
Katibu wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wa Wilaya hiyo,
Newton Mongi na Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya wilaya hiyo, Richard
Tiboche kwa tuhuma za kuikashifu Serikali na kuchochea mgogoro wa mpaka
kati ya hifadhi ya Serengeti na vijiji jirani.
Dk.
Kigwangalla ametoa agizo hilo jana majira ya saa tatu usiku baada ya
kuhitimisha ziara yake wilayani humo iliyolenga kutafuta suluhu ya
mgogoro uliodumu kwa miongo kadhaa kuhusu mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti na vijiji jirani ikiwemo kijiji cha Kegonga.
Akiwa njiani majira ya saa tatu za usiku kwenye
gari la wazi baada ya kukagua eneo hilo la mpaka kwa zaidi ya masaa
sita, Waziri Kigwangalla na msafara wake walikuta lundo la mawe yakiwa
barabarani ndani ya eneo la hifadhi hiyo, hali iliyosababisha taharuki
kubwa na msafara wake kushuka na kuanza kuondoa mawe hayo ili kupata
njia ya kupita.
Wakati
zoezi hilo likiwa linaendelea, Kiongozi huyo wa UVCCM alisikika
akiituhumu Serikali kwa kuweka mawe hayo na kwamba hayakuwekwa na
wananchi wa eneo hilo, jambo lililozua mshangao mkubwa kwa viongozi wa
Serikali waliokuwepo katika msafara huo akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mara,
Adam Malima.
Mkuu
huyo wa mkoa alisema tukio hilo sio la mara ya kwanza na kwamba
limewahi kuripotiwa mara nyingi na uongozi wa hifadhi hiyo kuwa wananchi
wa vijiji jirani hujaza mawe barabarani kwa ajili ya kuzuia magari ya
doria ili waweze kulisha mifugo yao ndani ya hifadhi hiyo. Alisema hata
msafara wa tume ya Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda iliyoundwa na CCM
hivi karibuni kufuatilia mgogoro katika eneo hilo nao ulizuiliwa kwa
mawe barabarani.
Imedaiwa
pia kuwa kwa nyakati tofauti viongozi hao wamekuwa wakiwatolea viongozi
wa Serikali maneno ya kejeli pamoja na kuwakwamisha kutekeleza majukumu
yao ya kuwahudumia wananchi ipasavyo.
Awali,
kabla ya tukio hilo la mawe barabarani moja ya gari lililokuwa
likiongoza msafara huo lilipata pancha baada ya kukanyaga misumari
iliyokuwa imetengwa kwenye moja ya barabara zinazoingia na kutoka ndani
ya Hifadhi ya hiyo ya Serengeti.
Waziri
Kigwangalla alisikitishwa na kitendo hicho ambacho alikielezea kuwa sio
cha kiuungwana kwa kuwa kinalenga kudhoofisha juhudi za Serikali
kumaliza mgogoro huo kwa faida ya pande zote.
"Mimi
ni Muislam, nimesikia kwa masikio yangu na wala sijaambiwa na mtu
yeyote na siwezi kumsingizia mtu, nimeshangazwa sana na kiongozi tena
mtendaji wa chama tawala anawezaje kuitukana Serikali, na hapa sisi
tumekuja kuwahudumia wananchi" alisema Dk. Kigwangalla kwa masikitiko
makubwa.
Wakati
huo huo, Waziri Kigwangalla ametoa miezi mitatu kwa wananchi wote
waliovamia ndani ya Hifadhi ya Serengeti na eneo la wazi (buffer zone)
ambao wanaendesha shughuli zao ikiwemo kilimo, ufugaji na makazi kuachia
maeneo hayo kwa hiari yao wenyewe, na kwamba muda huo ukipita
wataondolewa kwa nguvu na chochote kitakachokutwa ndani ya eneo hilo
kitatekezwa kwa mujibu wa sheria.
Akizungumzia
kuhusu suluhu ya mgogoro huo wa mpaka amesema, Serikali itaunda timu ya
wataalam kutoka wizarani kwake, wizara ya ardhi, uongozi wa mkoa wa
Mara na wilaya ya Tarime ambao watashirikiana na watu wengine huru
watakaochaguliwa na wananchi wa vjiji husika wakiongozwa na mbunge wao,
John Heche ambao watakuwa na uelewa wa kusoma ramani na kutafsiri mipaka
ili kushirikiana kuhakiki mipaka halisi ya eneo hilo na kufikia
muafaka.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kulia), Mkuu wa Mkoa wa
Mara, Adam Malima (kushoto) na viongozi wengine wa mkoa huo wakiangalia
mawe yaliyowekwa njiani kuzuia msafara wake kutoka ndani hifadhi ya
Serengeti na watu wasiojulikana wakati wa ziara yake ya kutatua mgogoro
wa mpaka kati ya hifadhi hiyo na vijiji jirani jana usiku.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, viongozi wa mkoa wa
Mara na wananchi wa vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti wakikagua eneo la mpaka lenye mgogoro kati ya vijiji na
hifadhi hiyo wakati wa ziara yake ya siku moja katika wilaya ya Tarime
mkoani Mara jana.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiteta jambo na Mbunge
wa Tarime John Heche wakati wa ziara yake ya kutatua mgogoro wa mpaka
kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani katika wilaya ya
Tarime mkoani Mara jana.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa eneo lenye
mgogoro wa mpaka kati ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji jirani
na Mbunge wa Jimbo la Tarime, John Heche wakati wa ziara yake ya kutatua
mgogoro huo mkoani Mara jana. Katikati aliyeinama ni Mkuu wa Mkoa huo,
Adam Malima.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, viongozi wa mkoa wa
Mara na wananchi wa vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti wakikagua eneo la mpaka lenye mgogoro kati ya vijiji na
hifadhi hiyo wakati wa ziara yake ya siku moja katika wilaya ya Tarime
mkoani Mara jana.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, viongozi wa mkoa wa
Mara na wananchi wa vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti wakikagua eneo la mpaka lenye mgogoro kati ya vijiji na
hifadhi hiyo wakati wa ziara yake ya siku moja katika wilaya ya Tarime
mkoani Mara jana.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akisoma taarifa
mbalimbali kuhusu mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji
jirani vya wilaya ya Tarime mkoa wa Mara wakati wa ziara yake ya siku
moja katika wilaya ya Tarime mkoani Mara kwa ajili ya kutatua mgogoro wa
mpaka kati ya vijiji na hifadhi hiyo jana. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa
Mara, Adam Malima na Mbunge wa Jimbo la Tarime, John Heche.
Post a Comment