Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akimkabidhi Mcheza Golf
mashuhuri zaidi duniani, Jack William Nicklaus wa nchini Marekeni zawadi
ya kinyago cha Makonde walipoagana katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Mwalimu J.K Nyerere Jijini Dar es Salaam baada ya kuhitimisha ziara
yake ya siku 10 ya kutembelea vivutio vya utalii hapa nchini.
Na Hamza Temba-WMU
.............................. .............................. ............
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla amesema Serikali
itatumia fursa ya ujio wa Mcheza Golf mashuhuri zaidi duniani, Jack
William Nicklaus kutoka nchini Marekeni kubuni viwanja vya mchezo huo
karibu na maeneo ya vivutio vya utalii nchini ili kuvutia watalii wengi
wa kimataifa na hivyo kukuza pato la sekta hiyo.
Dk.
Kigwangalla amesema hayo jana mara baada ya kumuaga mchezaji huyo
katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Jijini Dar es
Salaam alipokuwa akirudi nchini kwao baada ya kumaliza ziara yake ya
siku kumi yeye na familia yake katika vivutio mbali mbali vya utalii
hapa nchini.
“Tutatumia
utaalamu na uzoefu wake kwenye mchezo wa Golf kwa kumtaka aje na
kampuni yake atusaidie kutengeneza plan (mpango) ya kujenga viwanja vya
golf.
“Amedesign
viwanja zaidi ya 300 kwenye nchi zaidi ya 50 duniani na nchi hizo
zimefaidika, amesema katika project zake zaidi ya asilimia 90 zinafanya
vizuri pamoja na kwamba ni uwekezaji wa gharama kubwa bado imelipa kwa
kiasi kikubwa na hakuna hata kiwanja kimoja kimepata hasara na vimekuwa
vinasaidia kukuza utalii katika nchi hizo.
“Lengo
letu ni kutengeneza ukanda maalum wa viwanja vya golf ambao utakuwa na
viwango vya kimataifa na utavutia wacheza Golf kutoka nchi mbalimbali
duniani, kwahiyo hii ni aina nyingine ya utalii wa watu wenye uwezo
ambao wataleta pesa nyingi kwa wakati mmoja.
“Tutaendelea
kuwa na mawasiliano nae na kampuni yake ili tuweze kuona anawezaje
kutusaidia na sisi walau tuwe na hiyo plan (mpango) lakini pia tukapata
wawekezaji wakaja kuwekeza kwenye viwanja vya golf vitakavyojengwa
karibu na fukwe, karibu na mito au hifadhi za Taifa ambapo tutavutia sio
tu watalii ambao wanaokuja kufanya utalii wa wanyamapori au beach
lakini tutavutia watalii wanaokuja mahsusi kwa kwa ajili ya utalii wa
golf” alisema Dk. Kigwangalla.
Wakati
huo huo Dk. Kigwangalla amesema Serikali itaendelea kuheshimu na kujali
maslahi ya wageni mashuhuri wanaokuja nchini ikiwemo ya usiri wa safari
zao na kwamba atakayetaka aje kimya kimya na aondoke kimya kimya
atapata heshma hiyo na atakayekubali kuwa wazi naye pia atapata heshma
hiyo.
Kwa
upande wake Jack Nicklaus alisema amefurahishwa sana na vivutio
mbalimbali vya utalii alivyovishuhudia katika safari yake hapa nchini
pamoja na ushirikiano na ukarimu mzuri kutoka kwa watanzania na ameahidi
kuwa balozi wa utalii wa Tanzania huo aendako.
Jack
Nicklaus ndiye mchezaji mwenye tuzo nyingi kuliko wachezaji wengine wa
mchezo huo hapa duniani kwa sasa, ameweka rekodi ya kushinda mashindano
ya kulipwa 117 na mashindano makubwa 18 (major champions).
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiagana na Mcheza Golf
mashuhuri zaidi duniani, Jack William Nicklaus wa nchini Marekeni katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Jijini Dar es
Salaam baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku 10 ya kutembelea vivutio
vya utalii hapa nchini.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiwa na Mcheza Golf
mashuhuri zaidi duniani, Jack William Nicklaus wa nchini Marekeni katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K Nyerere Jijini Dar es
Salaam muda mfupi kabla ya kuondoka kurudia kwao baada ya kuhitimisha
ziara yake ya siku 10 ya kutembelea vivutio vya utalii hapa nchini.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla na Mcheza Golf mashuhuri
zaidi duniani, Jack William Nicklaus wa nchini Marekeni wakitumbuizwa
na kikundi cha ngoma katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu J.K
Nyerere Jijini Dar es Salaam muda mfupi kabla ya kuondoka kurudia kwao
baada ya kuhitimisha ziara yake ya siku 10 ya kutembelea vivutio vya
utalii hapa nchini.
Picha ya pamoja ya Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla, Mcheza Golf mashuhuri
zaidi duniani, Jack William Nicklaus wa nchini Marekeni na familia yake
na uongozi wa Bodi ya Utalii Tanzania ukiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi,
Jaji Mst. Thomas Mihayo muda mfupi kabla ya ugeni huo kuondoka na kurudi
kwao.
Post a Comment