Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wa tatu kutoka kulia akiwa na wakuu wa wilaya mbalimbali zilizopo mkoani Arusha mara baada ya kuwaapisha wakuu wapya wa wilaya za Arumeru na Longido |
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo amewataka wakuu wapya wa wilaya za Arumeru na longido kuhakikisha wanatekeleza wajibu wao kwa kuzingatia ilani ya chama cha mapinduzi na ahadi za mheshimiwa Raisi Magufuli na kamwe wasitumie nafasi yao kumuonea mtu.
Akizungumza mara baada ya kuwaapisha wakuu hao wapya wa wilaya za Arumeru (Jerry Murro) na Longido ( Frank James Mwaisumbe) amesema kuwa wakuu hao wa wilaya wamepewa jukumu kubwa na wanaheshima kubwa ambayo wanawajibika kuilinda kwa maslahi mapana ya nchi.
"Mmepewa
majukumu makubwa kuna tabia ukipewa nafasi unaona kubwa ikizoea unaona
ya kawaida mjuwe hii awamu ni tofauti lazima utendaji wenu uendane na
katiba,sheria na miongozo ya serikali" alisema.
Alisema
kuna watu wakiteuliwa wanajiona wana akili sana kuliko wanaowaongoza
hivyo,katika ofisi kuna watu wa kuwasaidia hakuna ambaye hana kazi
ofisini muwaheshimu ambao mtawakuta.
Mkuu
mpya wa wilaya ya Arumeru, Jerry Muro,amewataka viongozi wilaya ya
Arumeru ambao wanaona hawawezi kutekeleza Ilani ya uchaguzi ya Chama cha
Mapinduzi (CCM) wapishane kabla ya hajaingia ofisini.
Akizungumza
mara tu baada ya kuapishwa na Mkuu wa mko wa Arusha,Mrisho Gambo,Muro
alisema ambao watakaoshindwa kutekeleza Ilani watapata taabu sana.
"Najua Rais John Pombe Magufuli anataka nini, nitashangaa kama watajitokeza watu wachache kutupinga" alisema
Muro alisema, miaka miwili iliyobaki anataka kuidhihirishia Arumeru ,Arusha na Tanzania inakwenda kubadilika.
"Nakuja Arumeru kuwatumikia na hii(Ilani ya uchaguzi) ndio nakuja kuitekeleza" alisema
Muro amemshukuru,Rais John Magufuli kwa kumuamini na kumpa dhamana ya kwenda kuwatumikia wananchi wa Arumeru.
Alisema Rais John Magufuli ni zawadi na baraka kutoka kwa mungu kwani ndani ya muda mfupi amefanya mambo mengi makubwa .
Kwa
upande wake,Mkuu mpya wa wilaya ya Longido,Frank James Mwaisumbe
alimshukuru Rais Magufuli kwa kimteua na kuahidi kufanyakazi kwa nguvu
zake zote,jasho lake na damu yake.
Mwaisumbe alisema amekuja kuweka chache ya maendeleo Longido pale ambapo wenzake wameishia ataendeleza.
"Nafahamu tayari mmefanya mengi mimi nimekuja kuendekeza na kuweka nguvu na kujifunza " alisema
Post a Comment