PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: TANAPA, NCAA NA CFC ZACHANGAMKIA FURSA NANENANE KUTANGAZA UTALII NA KUPINGA VITA UJANGILI
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
    Maonesho ya wakulima na wafugaji nane nane mwaka 2018,yanatumiwa na Taasisi za uhifadhi kutangaza vivutio vya Utalii nchini na...

 
 
Maonesho ya wakulima na wafugaji nane nane mwaka 2018,yanatumiwa na Taasisi za uhifadhi kutangaza vivutio vya Utalii nchini na kupiga vita ujangili.


Taasisi za uhifadhi,Shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA),Friedkin conservation Fund (FCF) na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro,wameeleza ushiriki wao katika maonesho ya mwaka huu.

Akizungumza mapema leo,Meneja kitengo cha ujirani Mwema cha shirika la hifadhi za Taifa(TANAPA),Ahmed Mbugi alisema shirika hilo limejipanga kutumia maonesho haya kutangaza utalii.

Mbugi alisema katika maonesho hayo,TANAPA itatoa magari kuwapeleka watalii hifadhi za taifa za Serengeti kwa washiriki wa maonesho ya kitaifa mkoani Simiyu.

Alisema kwa wanaoshiriki maonesho mkoa wa Morogoro watapelekwa Hifadhi ya Taifa ya mikumi kwa kuchangia gharama.

Katika maonesho hayo,pia Taasisi binafsi za uhifadhi zitatoa huduma ikiwepo taasisi ya Friedkin conservation Fund(FCF) ambayo kwa mara ya kwanza itashiriki.

Mkurugenzi wa kampuni ya Mwiba Holdings, moja ya kampuni zilizo chini ya FCF ,Abdukadir Mohamed alisema katika maonesho mwaka huu wameandaa mabanda ambayo watatoa elimu ya uhifadhi na vita dhidi ya ujangili.

"Pia tutahamasisha watanzania kwenda kutembelea vivutio vya utalii katika mapori ya akiba  ambayo tumewekeza ikiwepo eneo la makao kwa wakazi wa kanda ya ziwa" alisema

Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro(NCAA) pia wanatumia maonesho kupeleka watalii wa ndani kuona vivutio vilivyopo Ngorongoro.

Naibu Mhifadhi Mkuu wa Ngorongoro,Dk Maurus Msuha alisema magari maalum yameandaliwa kutoka Arusha hadi Ngorongoro kutembelea vivutio kwa malipo kidogo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top