Waziri
wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza
na wadau wa Kahawa Wilayani Muleba wakati wa ziara ya siku tatu ya
kikazi Mkoani Kagera, Jana 12 Julai 2018. (Picha Zote Na Mathias Canal-WK)
Waziri
wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la
Muleba kusini Mhe. Prof Anna Tibaijuka kabla ya mkutano na wadau wa
Kahawa Wilayani Muleba wakati wa ziara ya siku tatu ya kikazi Mkoani
Kagera, Jana 12 Julai 2018.
Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage akimakabidhi
muongozo wa ujenzi wa viwanda Mkuu wa Wilayani ya Muleba Mhe Richard
Ruyango mara baada ya kuwasili Wilayani humo kwa ajili ya mkutano wa
wadau wa Kahawa wakati wa ziara ya siku tatu ya kikazi Mkoani Kagera,
Jana 12 Julai 2018. Mwingine pichani ni Mkurugenzi wa viwanda vidogo na
biashara ndogo kutoka Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt
Consolata Ishebali.
Waziri
wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati akizungumza
na wadau wa Kahawa Wilayani Muleba wakati wa ziara ya siku tatu ya
kikazi Mkoani Kagera, Jana 12 Julai 2018.
Na Mathias Canal-WK, Muleba-Kagera
Waziri
wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba Jana 12 Julai 2018 ameitaka Benki ya
CRDB kulipa haraka malipo ya fedha za Ushirika za Chama Kikuu cha Kagera
(KCU) kulingana na hatma ya kesi iliyokuwa mahakamani mwaka 2003 ambapo
wakulima walikuwa wakikatwa kiasi cha shilingi 10 kwa kila kilo moja ya
Kahawa ili kujenga mfuko wa Mazao kwa miaka mitatu kuanzia mwaka 1990
hadi 1993.
Dkt
Tizeba ametoa agizo hilo wakati akizungumza kwenye mkutano
uliowakutanisha wadau wa Kahawa Wilayani Muleba ikiwa ni siku ya tatu ya
ziara ya kikazi mkoani Kagera iliyoanza Juzi 10 Julai 2018 na
kuhudhuriwa pia na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe Charles
Mwijage.
Swala
la madai hayo katika mkutano huo liliibuka baada ya baadhi ya wakulima
kuonyesha vitabu vya mfuko huo ambapo makato hayo ya shilingi 10 kwa
kilo kwa kipindi cha miaka mitatu jinsi ambavyo yalikuwa yakifanyika.
Madai
ya wakulima hao yamekuwa yakilalamikiwa kwa kipindi kirefu na kuchangia
kwa kiasi kikubwa kupungua kwa imani ya wakulima kwa chama kikuu cha
ushirika Kagera (KCU).
Chanzo
cha kesi hiyo ni baada ya Benki ya CRDB kuzuia fedha za malipo
yaliyotokana na mauzo ya Kahawa ili kulipia deni la msimu wa mwaka
1997/1998.
Hukumu
ya kesi iliyotolewa tarehe 28 Octoba 2009 na mfuko wa Mazao wa wakulima
Mkoani Kagera kupewa tahfifu ulizoomba ambapo tangu wakati huo Benki ya
CRDB iliweza kulipa fedha za mfuko ilizochukua kiasi cha shilingi
milioni 525 na fedha zilizobaki bado hazijalipwa kwa kisingizio cha kuwa
na nia ya kukata rufaa ambayo bado haijakatwa ambapo hata hivyo
hawawezi kukata rufaa kutokana na muda kuwa umepita.
Dkt
Tizeba alisema kuwa Jumla ya madai hayo sambamba na riba ni shilingi
Bilioni sita za kitanzania huku akisisitiza kuwa Benki hiyo ya CRDB
inapaswa kuwa mfano wa Benki zingine nchini hivyo kushindwa kuwalipa
wakulima kwa wakati ni kushindwa kwenda na serikali ya awamu ya tano
inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John
Pombe Magufuli.
Post a Comment