PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: BODI YA WAKURUGENZI TAWA YARIDHISHWA NA UWEKEZAJI WA MWIBA HOLDING NA TGTS KATIKA UHIFADHI ENEO LA MAKAO WILAYANI MEATU
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
NA: ANDREA NGOBOLE, PMT Bodi ya wakurugenzi ya mamlaka ya usimamizi wanyamapori nchini (TAWA) imeridhishwa n...










NA: ANDREA NGOBOLE, PMT

Bodi ya wakurugenzi ya mamlaka ya usimamizi wanyamapori nchini (TAWA) imeridhishwa na utendaji wa Makampuni ya uwindaji na upigaji picha za kitalii, ya Mwiba holdings na TGTS yaliyowekeza katika pori la akiba Makao, lilipo mpakani mwa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na Meatu.

Wanyama wameongezeka, vita dhidi ya ujangili imefanikiwa na mifugo imedhibitiwa kuingia maeneoya hifadhi lakini pia uchangiaji wa fedha za maendeleo umeongezeka.

Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa bodi ya TAWA,Meja Jenerali  mstaafu Hamisi Semfuko alipotembelea maeneo yaliyowekezwa na kampuni ya mwiba katika eneo la Makao na kitalu Mbono kinachomilikiwa na kampuni ya TGTS.

Amesema kuwa wanyama wameongezeka katika vitalu hivyo vilivyopo wilayani Meatu kutokana na ushirikiano kati ya wawekezaji hao na askari wa Tawa.

Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya  Usimamizi wa Wanyamapori nchini (TAWA), Dk James Wakibara akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, juu ya mchango kwa jamii, uhifadhi na kiuchumi wa  makampuni ya uwindaji wa kitalii umekuwa na msaada mkubwa kwa maendeleo ya jamii ambapo zimechangia zaidi ya shilingi bilioni 40.

Dk Wakibara alisema, licha  mchango wa makampuni kwenye jamii, pia TAWA kupitia malipo  ya kampuni hizo, imekuwa ikitoa  takriban sh 6.5 bilioni kila mwaka kwa vijiji vyenye wawekezaji hao na halmashauri.

Makampuni hayo yamewekeza katika baadhi ya maeneo ya vitalu 159   vilivyopo nchini na maeneo ya hifadhi za jamii za wanyamapori (WMA) 38 zilizopo nchini.

"Hizi kampuni za kitalii zina mchango mkubwa sana pia katika uhifadhi wa maeneo haya, hasa katika vita dhidi ya ujangili ikizingatiwa asilimia 95 ya maeneo yaliyohifadhiwa nchini yapo chini ya TAWA"alisema

Alisema kwa sasa mapato ya TAWA kutokana na shughuli za uhifadhi, yamefikia dola 20 lakini kuna mikakati ya kuongeza mapato hayo mara nne zaidi hadi kufikia dola 80.

"kuna dhana potofu kuwa uwindaji wa kitalii ni kumaliza wanyama hili sio kweli, kwani haya makampuni hayajawahi kufikia hata robo  kiwango cha kuwinda wanyama ambacho kinatolewa kila mwaka na TAWA na mashirika ya kimataifa"alisema

Mwenyekiti wa bodi ya TAWA,Meja Jenerali  mstaafu Hamisi Semfuko alisema mamlaka hiyo ipo katika mabadiliko  makubwa ili kuhakikisha jamii inanufaika zaidi ya uhifadhi wa wanyamapori,katika kusaidia miradi ya kijamii ya maji, afya Elimu na uhifadhi.

Mwenyekiti huyo na bodi yake ambao walitembelea pori la Makao, lilipo mpakani mwa Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro na Meatu,alisema wameridhishwa na utendaji wa kampuni ya Mwiba Holding katika eneo hilo.




Kampuni ya Mwiba holding imewekeza katika hifadhi ya jamii ya wanyamapori(WMA) ya makao na katika eneo la ranchi katika kijiji cha makao wilayani Meatu.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top