Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Mrisho
Gambo amezindua bodi mpya ya saba ya Parole mkoa wa Arusha na kuitaka
bodi hiyo kufanyakazi kwa weledi pindi wanapokuwa wakitekeleza majukumu
yao na kuepuka upendeleo wakati wa kutoa msamaha kwa wafungwa
Akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa bodi hiyo
yenye wajumbe zaidi ya 10 katibu tawala wa mkoa huo,Richard Kwitega
akimwakilisha mkuu huyo wa mkoa amesema kuwa bodi hiyo ina manufaa
makubwa kwa taifa iwapo itatimiza majukumu yake ipasavyo bila kuwa na
upendeleo unaotokana na vitendo vya rushwa
'Msikubali kupitisha wafungwa wasiokuwa na vigezo vinavyotakiwa bali tutafute wanufaika halisi wa parole "Amesema Kwitega
Ameongeza kuwa iwapo bodi hiyo itatekeleza kwa weledi itaisaidia kupunguza msongamano kwa wafungwa na kuisaidia serikali katika kupunguza gharama za kuhudumia wafungwa.
Awali Mwenyekiti wa bodi hiyo ya Parole ,David Marandu
Pamoja na kumpongeza waziri wa mambo ya ndani kwa uteuzi wa bodi
hiyo amesema watahakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa kujua kwamba
kazi hiyo ni ngumu na inahitaji umakini wa hali ya juu.
Amesema jeshi la magereza ambao ndio wanaoishi na kuangalia wafungwa wahakikishe wanawaletea wafungwa wenye sifa ili kuirahisishia bodi hiyo katika kutekeleza majukumu yake bila upendeleo.
"Siwezi kushukuru jambo hili kwamba tumepewa kazi jepesi bali tuamini kwamba kazi hii ni ngumu na tuifanye kwa weledi kwa kuwa inahusu maisha ya watu'Amesema
Naye Kamishina msaidizi mwandamizi wa jeshi la Magereza mkoa wa Arusha (SACP),Hamis Mkubasi ,amesema wanufaika wa mpango wa parole ni wale wenye vifungo virefu kuanzia miaka minne na kuendelea.
Ila wale wenye makosa yanayohusu hisia ya jamii kama.vile unyang'anyi wa kutumia silaha ,ubakaji ,ulawiti na mauaji hawatakuwa sehemu ya mpango huo wa parole.
Amesema sifa mojawapo kwa mfungwa itakayompa msamaha wa oarole ni pamoja na kutumikia kifungo kwa theluthi moja akiwa gerezani,kuwa na heshima gerezani, Kuishi kwa kufuata sheria na asiwe alishawahi kupata msamaha wa parole.
Amesema katika kipindi cha miaka minne katika gereza kuu Arusha wametoa msamaha kwa wafungwa 63 kati ya 65 waliopendekezwa huku Wawili wakikosa sifa.
Post a Comment