Kiongozi wa mbio za mwenge Kitaifa, Charles Kabeho amegoma
kuzindua mradi wa ujenzi wa nyumba za watumishi wa halmashauri ya
Kalambo mkoani Rukwa kwa madai kuwa thamani ya fedha za ujenzi
zilizotumika haziendani na nyumba hizo.
Tukio hilo limetokea Mei 8,2018 baada ya kiongozi huyo
kutembelea mradi huo wakati mwenge wa Uhuru ukikimbizwa wilayani
Kalambo huko mkoani Rukwa.
Hata hivyo kiongozi huyo ameitaka Taasisi ya Kuzuia na
Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuchunguza mradi huo unaotajwa kuwa na
thamani ya Sh511 milioni, akibainisha kuwa kuna matumizi mabaya ya fedha
za umma.
Kwa mujibu wa taarifa ya ujenzi huo uliyotolewa na
mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Kalambo, Simon Kagani amesema kuwa
mradi huo ulianza kutekelezwa Julai 2016 na kukamilika Aprili 2017 na
kugharimu kiasi hicho cha fedha, ambapo Serikali Kuu imechangia
Sh496milioni, halmashauri Sh15milioni.
Post a Comment