PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MKUTANO MKUU WA 23 WA BENKI YA CRDB WAFANYIKA JIJINI ARUSHA, WANAHISA WAMTAKA DKT. KIMEI KUENDELEA KUIONGOZA BENKI YAO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
TAASISI za fedha hasa mabenki yanakabiliwa na ushindani mkubwa kutokana na ongezeko la huduma za kifedha kutolewa na makampuni ya simu. ...
TAASISI za fedha hasa mabenki yanakabiliwa na ushindani mkubwa kutokana na ongezeko la huduma za kifedha kutolewa na makampuni ya simu.

Suala hilo limechangia kwa kiasi kikubwa kufungwa kwa benki tano, huku nyingine tano zikiwa chini ya uangalizi maalumu.

Ili kukabiliana na ushindani huo, Benki ya CRDB imejipanga kukabiliana na ushindani huo kwa mwaka 2018 ili kuona inapata ufanisi. Na hiyo pia ni kutokana na Serikali kutoa fursa kadhaa kwa mabenki nchini kujiendesha kwa faida.

Hayo yamesemwa leo Mei 19, 2018 na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Dkt. Charles Kimei wakati anasoma taarifa yake kwenye Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki hiyo uliofanyika Ukumbi wa Simba (AICC) jijini Arusha.

"Kutokana na ushindani mkali kutoka taasisi zisizo za kifedha, hasa huduma za simu za mkononi na changamoto nyingine, benki nyingi ndogo zilikuwa na hali ngumu, na benki takribani tano zilifungwa na Benki Kuu, na benki nyingine tano ziliwekwa chini ya uangalizi maalumu.

"Ili kukabiliana na changamoto za ukwasi na kuongeza kasi ya ukuaji wa mikopo kwa sekta binafsi, Benki Kuu ilipunguza kiwango cha amana ya benki hadi kufikia asilimia nane (8) na kupunguza kiwango cha riba kwa mikopo ya benki za biashara kutoka asilimia 12 hadi tisa" alisema Dkt. Kimei.

Dkt. Kimei alisema kwa maana hiyo benki za biashara zina uwezo wa kukopa fedha hizo serikalini na wao kuweza kuwakopesha wafanya biashara na watu binafsi, hivyo kurudisha mzunguko wa fedha na shughuli za kawaida kwa wananchi.

Hivyo, Benki ya CRDB imejiwekea malengo ya kimkakati kwa mwaka 2018. Mpango mkakati huo wa miaka mitano 2018-2022, una lengo la kuifanya benki ya CRDB na kampuni zake tanzu kuongoza katika kupata faida kwa kukuza ubora wa rasilimali kupitia huduma kwa wateja.

Wateja hao ni wale binafsi, wadogo na wa kati, ikitumia huduma za kidijitali zenye ubora wa hali ya juu, huku wakiahidi kufanya mageuzi makubwa mwaka huu, katika matawi yao kwa lengo la kuongeza ufanisi na tija.

"Lengo kuu mwaka 2018 litakuwa ni kuongeza kasi ya mageuzi ya kidijitali na kupunguza kiwango cha mikopo chefuchefu (isiyo rudishwa kwa wakati) hadi asilimia nane, kuboresha wastani wa kiwango cha gharama na mapato hadi asilimia 58, na kufanya mageuzi ya uendeshaji kwenye matawi ya benki ili kuongeza tija na ufanisi" alisema Dkt. Kimei.
MMG_6443
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei akizungumza wakati akitoa taarifa ya Benki kwa Wanahisa wa Benki hiyo, katika Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Simba uliopo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini Arusha  Mei 19, 2018. Katika Mkutano huo, Sehemu kubwa ya wajumbe wamemuomba Mkurugenzi Mkuu wa Benki hiyo,  Dkt. Charles Kimei kuendelea kuitumikia nafasi yake hiyo, ya kuingoza benki hiyo kwa miaka mingine mitano. 

Hatua hiyo ilifikia pindi, Dkt. Kimei alipowajulisha wanahisa hao wakati alipokuwa akitoa hotuba ya mwenendo wa benki, kuwa kwenye mkutano mkuu ujao, atawaaga rasmi baada ya kumaliza muda wake wa kuitumia Benki hiyo.

Kwenye michango yao, baadhi ya wanahisa hao walisema hiki ni kipindi kigumu kiuchumi hivyo CRDB inahitaji mtu mwenye uzoefu wa kutosha kukabiliana na changamoto zilizopo. Mmoja wa wanahisa hao, Emburis Sirikwa wa Arusha alisema endapo mkurugenzi huyo ataondoka na kuiacha benki hiyo, ndani ya miaka miwili ya kutokuwanaye lazima ufanisi utapungua.
MMG_6181
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Ally Laay akizunguza katika Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, unaofanyika kwenye Ukumbi wa Simba uliopo katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini Arusha  Mei 19, 2018. 
MMG_6168
Mwenyekiti wa Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, Abeid Mwasajone akizungumza jambo kwa wajumbe wa Mkutano huo, unaofanyika  Mei 19, 2018 kwenye Ukumbi wa Simba uliopo ndani ya Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha AICC, Jijini Arusha.
MMG_6371
MMG_6379
MMG_6390
MMG_6401
MMG_6405
 Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, wakiwa kwenye Mkutano huo, unaofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini Arusha  Mei 19, 2018.
MMG_6075
Katibu wa Benki ya CRDB na Mkurugenzi wa Maswala ya Kampuni, John Rugambo akizungumza wakati akifungua Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, unaofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini Arusha  Mei 19, 2018.MMG_6256

MMG_6503
MMG_6551
MMG_6561
MMG_6537
Sehemu ya Wanahisa wa Benki ya CRDB wakichangia mada mbalimbali zinazoendelea kutolewa katika Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, unaofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini Arusha  Mei 19, 2018.
MMG_6114
Mtangazaji wa zamani wa Radio Tanzania na Mwanahisa wa Benki ya CRDB, Mzee Salim Mbonde akichangia mada katika Mkutano Mkuu wa 23 wa Wanahisa wa Benki ya CRDB, unaofanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa (AICC), jijini Arusha  Mei 19, 2018.
MMG_6321

MMG_6322

MMG_6323

MMG_6334

MMG_6483

MMG_6489

MMG_6502


MMG_6512

MMG_6513

MMG_6525

MMG_6529

MMG_6533

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top