Mkuu wa Jeshi
la Polisi, IGP Simon Sirro amemteua Naibu Kamishna wa Polisi, Maulid Makabila
kuwa Naibu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (D/DCI) Zanzibar, huku akifanya
mabadiliko ya baadhi ya makamanda wa polisi wa mikoa
Kabla ya
uteuzi huo, Makabila alikuwa mkuu wa kitengo cha kuzuia uhalifu makao makuu ya
Polisi Dar es Salaam
Taarifa
iliyotolewa Alhamisi Mei 17, 2018 na msemaji wa polisi, Barnabas Mwakalukwa
imeeleza kuwa katika mabadiliko hayo aliyekuwa DCI Zanzibar, Ramadhan Ng’anzi
ameteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha kuchukua nafasi ya Charles
Mkumbo aliyehamishiwa makao makuu ya upelelezi, Dar es Salaam
Aliyekuwa
kamanda wa polisi Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan Nassir Ali anakwenda kuwa
kamanda wa polisi Mkoa wa Kaskazini Pemba. Nafasi yake imechukuliwa na Kamishna
Msaidizi wa polisi, Thobias Sedoyeka aliyekuwa makao makuu ya upelelezi Dar es
Salaam
“Kamanda
wa polisi mkoa wa Kusini Unguja, Makarani Khamisi amehamishiwa makao
makuu ya upelelezi Zanzibar na nafasi yake kuchukuliwa na kamishna msaidizi wa
polisi, Suleiman Hassan aliyekuwa mkuu wa upelelezi Mkoa wa Kaskazini Unguja,”
anasema Mwakalukwa katika taarifa hiyo
Aliyekuwa
kamanda wa polisi Mkoa wa Kaskazini Unguja, Hasina Ramadhani Taufiq anakuwa
ofisa mnadhimu makao makuu ya polisi Zanzibar na nafasi yake inachukuliwa na
kamishna msaidizi, Haji Abdallah Haji aliyekuwa ofisa mnadhimu Mkoa wa Mjini
Magharibi.
Taarifa hiyo
inaeleza mabadiliko hayo ni ya kawaida yenye lengo la kuongeza ufanisi wa
utendaji kazi.
Post a Comment