PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: Zitto Kabwe Ajitolea Kumsindikiza Abdul Nondo Uhamiaji...Adai Kwenda Kuhoji kama Wakigoma sio Watanzaniia
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema Aprili 20 ataongozana na Mwanafunzi Abdul Nondo kupeleka vyeti vya kuzaliwa katika ofisi za ...
 
Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amesema Aprili 20 ataongozana na Mwanafunzi Abdul Nondo kupeleka vyeti vya kuzaliwa katika ofisi za Idara ya Uhamiaji kama alivyotakiwa kuthibitisha uraia wake

Zitto amesema yeye kama Mbunge wa Kigoma ambapo ndipo nyumbani kwa mwanafunzi huyo, ataruhusu wapiga kura wake kumsindikiza ili kuhoji kama Wanakigoma sio Watanzania maana kila mara wamekuwa wakihojiwa juu ya uraia wao

Abdul Nondo alifika Idara ya Uhamiaji mapema jana kuitikia wito ambapo baada ya mahojiano akaamriwa awasilishe cheti chake cha kuzaliwa pamoja na vya wazazi wake ifikapo tarehe 20 mwezi huu

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top