PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: NA HIVI NDIVYO MICHAEL WAMBURA ALIVYOTUA LEO OFISI ZA TFF...
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
MAPEMA Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura alilalamika kubaniwa haki yake ya kuk...

Image result for MICHAEL WAMBURA

MAPEMA Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Michael Wambura alilalamika kubaniwa haki yake ya kukataa rufaa baada ya kupatikana na hatia na kufungiwa maisha kujihusisha na soka.
Lakini leo ndiyo ile siku ambayo amekuwa akiisubiri kwa hamu kubwa na atakuwa na nafasi ya kusikilizwa.
Wambura amepanga leo kutinga katika ofisi za shirikisho hilo akiwa amejiandaa na yuko vizuri kwelikweli kujitetea kwenye Kamati ya Rufaa ya Maadili ya TFF ambayo inakutana leo Jumamosi.
Hatua hiyo imekuja baada ya Machi 15, mwaka huu, Kamati ya Maadili ya TFF kutangaza kumfungia Wambura kutojihusisha na masuala ya soka maisha yake yote baada ya kumkuta na makosa matatu.

Makosa hayo ni kupokea fedha za TFF malipo yasiyo halali, kughushi barua ya kuelekeza malipo ya Kampuni ya Jeck System Limited na kushusha hadhi ya shirikisho hilo.


Baada ya kutoka kwa hukumu hiyo, Wambura na wakili wake, Michael Muga, walikata rufaa ambayo leo Jumamosi itajadiliwa na kutolewa uamuzi.


Wambura alisema amejipanga kikamilifu kwenda kujitetea kutokana na kutoridhika na jinsi ishu yake hiyo ilivyoendeshwa.


“Nina kila sababu ya kujipanga kwenda kujitetea kwani naamini sikutendewa haki kwa sababu hakuna ushahidi wa kile ambacho nimetuhumiwa nacho,” alisema Wambura.

Naye Wakili Muga alisema, mteja wake huyo yupo tayari kwenda kujitetea na yeye ataendelea kuwa upande wake licha ya kuwepo kwa taarifa za kutakiwa ajiondoe baada ya TFF kuwasilisha barua kwenye Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) wakitaka asiendelee kumtetea.


“Mteja wangu yupo tayari kwa kujitetea na mimi nitaendelea kuwa upande wake kwa sababu TLS siyo kazi yao kumuambia wakili asimuwakilishe mteja na haijawahi kutokea,” alisema Muga.

  CREDIT: CHAMPIONI

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top