Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Kamishna
Msaidizi wa Ardhi kanda ya Kaskazini Leo Komba amesema kuwa serikali
itawachukulia hatua wamiliki wa ardhi wasiolipa kodi ya ardhi kwa mujibu wa sharia
ya ardhi Namba 4 ya mwaka 1999 hivyo amewataka kulipa kodi hiyo kwa wakati ili
kuepuka kufikishwa mahakamani.
Akizungumza
jijini Arusha Komba alisema kuwa wizara imejipanga kikamilifu kusimamia taratibu za kuwafikisha mahakamani
wadaiwa wote watakaokaidi kulipa kodi ya ardhi na kukusanya kodi ya pango la
ardhi kwa kila kipande cha ardhi kilichomilikishwa kwa mujibu wa sharia.
Aidha
alisema kuwa Wizara imerahisisha ulipaji wa kodi ya pango la ardhi ambapo
mmiliki akishapata Ankara ya madai anaweza kulipa kwa kutumia simu ya kiganjani
.
“Pamoja na
suala zima la ulipaji kodi la Ardhi ,Mhe.Waziri wa Ardhi ameanzisha kampeni ya
Funguka kwa Waziri wa ardhi kuondoa migogoro ya ardhi ,Hivyo wale wananchi
wenye kero za ardhi wanatakiwa kujaza fomu ambazo zipo kwenye ofisi zote za
Halmashauri na Ofisi za wakuu wa Wilaya ili Waziri atatue kero hizo” Alisema
Kamishna
Naye Afisa
Ardhi Mwandamizi Thadeus Riziki amesema
kuwa ardhi ambazo hutozwa kodi hiyo ni zile ardhi ambazo zimepimwa na zina
hatimiliki,maeneo ambayo hayajapimwa mengi hayajaingizwa katika mpango wa
kulipa kodi.
Afisa huyo
alisema kuwa serikali ina mpango wa kupima maeneo ambayo hayapimwa na pia
kurasimisha makazi holela ili waweze kupatiwa huduma muhimu za kijamii.
Alisema kuwa
ni vyema wananchi wakajijengea utaratibu wa kulipa kodi kwa wakati ili kuepuka
usumbufu ikiwemo kufikishwa mahakamani .
Post a Comment