Viongozi wa chama cha waongoza watalii wakifuatilia mada na maswali toka kwa wajumbe wa mkutano wa waongoza watalii uliofanyika katika ukumbi wa Manor Hotel mwishoni mwa juma hili |
Baadhi ya waongoza watalii wakisikiliza uwasilishwaji wa mada katika mkutano wao mkuu uliofanyika katika ukumbi wa Manor Hotel mwishoni mwa wiki |
Chama cha waongoza watalii nchini(TTGA), kimeombwa kuisaidia serikali kwa kutoa taarifa za baadhi ya kampuni za utalii ambazo zimekuwa zikikwepa kulipa kodi na ambazo hazilipi malipo stahiki kwa waongoza watalii.
Afisa Utalii ofisi za Mkuu wa mkoa wa Arusha.Flora Basir
alitoa wito huo, wakati akifungua mkutano mkuu wa TTGA na kueleza
Serikali inathamini kazi za waongoza watalii kwani ndio wamekuwa
wakiwapokea na kukaa muda mrefu na watalii lakini wanaweza kusaidia
kuzuia kukwepwa kodi.
"waongoza watalii ni mabalozi wetu wakubwa wautalii,
serikali inajua changamoto zenu na inazifanyia kazi, ikiwepo malipo duni
mnayolipwa lakini tunawaomba msaidie kutoa taarifa kwa wanaokwepa
kulipa kodi "alisema.
Awali Katibu Mkuu wa TTGA, Emmanuel Mollel alisema licha ya
wao kufanyakazi nzuri ya kuwapokea watalii na kuwasafirisha katika
hifadhi za taifa na maeneo mengine ya utalii,bado wanakabiliwa na
changamoto kadhaa.
Mollel alisema ,wanachangamoto ya kutokuwa na mikataba ya
kazi,malipo duni, huduma duni kwenye hoteli za hifadhini,kero ya malango
ya kuingia hifadhini, matatizo ya kukamatwa na askari wa usalama
barabarani wakiwa na watalii na utata wa leseni za kazi yao.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa TTGA, Khalifa Msangi, alisema
wanashukuru sana hatua ambazo zinaendelea kuchukuliwa na serikali
kutatua baadhi ya kero lakini kasi ni ndogo sana.
"hivi sasa Serikali inatambua kazi wetu na tunaushirikiano
lakini tungependa hizi kero zetu zipatiwe ufumbuzi ili serikali ifikie
lengo la kupata watalii milioni 5 ifikapo mwaka 2020 kwani sisi ndio
mabalozi wakubwa wa utalii"alisema
Akizungumza katika mkutano huo, Mhifadhi Utalii wa Hifadhi
za Taifa ya Serengeti, Susuma Kusekwa alisema, shirika la hifadhi za
Taifa(TANAPA) kwa kushirikiana na Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro(NCAA)
wameanza kufanyia kazi kero za waongoza watalii.
"kuna kero za kukamatwa ndani ya hifadhi kutokana na kupita
njia ambazo hazitakiwi hasa kuelekea eneo la Ndutu kwenye mazalia ya
Nyumbu tunalifanyia kazi na Serengeti tutajenga barabara mpya katika
eneo hilo"alisema
Hata hivyo, alitaka waongoza watalii hao, kufanyakazi kwa
waledi na wakati wote wanapokabiliwa na changamoto wawasiliane na
viongozi wa hifadhi ili kusaidiwa badala ya kulalamika tena wakiwa na
watalii.
Post a Comment