Mkurugenzi wa Taasisi ya Wanaume ya Men at work Maxwell Stanslaus akizungumza na Mkazi wa Arusha katika zoezi la uchangiaji wa damu lililoendeshwa ma taasisi yake.Picha na Ferdinand Shayo |
Mwanachama wa Taasisi ya Wanaume ya Men at work akichangia damu |
Mwanachama wa Taasisi ya Wanaume ya Men at work Rodgers Nelson akichangia damu katika viwanja vya Sheikjh Amri Abeid |
Wanachama wa Taasisi ya Wanaume ya Men at work Rodgers Nelson wakichangia damu katika viwanja vya Sheikjh Amri Abeid |
Na Ferdinand Shayo,Arusha.
Taasisi
isiyokua ya kiserikali ya Wanaume inayojulikana kama Men At Work imeendesha
zoezi la kuchangia damu kwa ajili ya kinamama wanaojifungua na kupoteza damu nyingi pamoja majuruhi
wanaonusurika na ajali na kufikishwa katika hospitali ya mkoa ya Mount Meru .
Mkurugenzi
wa Taasisi hiyo Maxwell Stanslaus amesema
kuwa wameamua kuwa wameamua kuchangia damu kama mchango wanaume kujitoa kwa ajili ya
jamii na kuisaidia jami kwasababu wanaume ni nguzo ya familia,jamii na taifa
kwa ujumla.
Max
aliwataka wanaume wote nchini kuwajibika na kuwa mstari wa mbele katika kutatua
changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii .
“Kwa sasa tumeamua kushirikiana na
kitengo cha damu salama kuchangia damu ili kupunguza changamoto ya upungufu wa
damu katika benki ya damu “ Alisema Max
Max alisema
kuwa taasisi hiyo ina kazi kuwa ya kuwahasisha wanaume kuwa wawajibikaji na
kushiriki katika nafasi za malezi familia na jamii ili kujenga familia imara na
hatimaye taifa imara.
Kwa upande
wake Mwanachama wa Men At Work Rodgers Nelson alisema kuwa anajisikia faraja
kuchangia damu ili kusaidia kuokoa
maisha ya kinamama wajawazito ambao hupoteza damu nyingi wakati wa kujifungua.
Naye Shemeji
Melayeki alieleza kuwa ni mara yake ya
kwanza kutoa damu hivyo amewatoa hofu wananchi kutokua waoga wa kuchangia damu
kwani zoezi hilo linafanyika kwa umakini na halina madhara yoyote.
Post a Comment