Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na balozi wa
Uingereza hapa nchini, Sarah Cooke ofisini kwake mjini Dodoma jana
ambapo walijadili mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano katika
sekta ya uhifadhi na maendeleo ya utalii.
Na Hamza Temba-Dodoma
.............................. .............................. ......
Serikali imefanikiwa kudhibiti vitendo vya ujangili hapa nchini kwa zaidi ya asilimia 50.
Hayo
yameelezwa jana na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi
Kigwangalla wakati akizungumza na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Sarah
Cooke ofisini kwake mjini Dodoma.
Mazungumzo
hayo yalilenga kujadili mambo mbalimbali ikiwemo kuimarisha ushirikiano
baina ya nchi hizo mbili katika sekta ya uhifadhi na maendeleo ya
utalii.
Dk.
Kigwangalla alisema katika kipindi cha miezi sita iliyopita hakuna
mauaji mapya ya wanyamapori yaliyoripotiwa na kwamba nyara zinazokamatwa
hivi sasa ikiwemo meno ya tembo na ngozi za wanyamapori ni masalia ya
zamani.
Amesema
mafanikio hayo yametokana na juhudi mbalimbali zinazofanywa na Serikali
kudhibiti vitendo vya ujangili ikiwemo doria za mara kwa mara za
kiitelijensia ambazo zimekuwa zikishirikisha vyombo mbalimbali vya
ulinzi na usalama pamoja na raia wema.
Alisema
Serikali itaendelea kudhibiti vitendo hivyo kwa kuimarisha ulinzi
katika maeneo ya hifadhi nchini ikiwa ni pamoja na kuanzisha jeshi
maalum la usimamizi wa Misitu na Wanyamapori, Sheria ya wanyamapori na
za taasisi za uhifadhi zimeanza kufanyiwa marekebisho kuwezesha
mabadiliko hayo.
Katika
hatua nyingine Dk. Kigwangalla amemueleza balozi Cooke kuwa, Serikali
kupitia Wizara yake inaendelea kuimarisha vivutio vya utalii hapa
nchini kwa kupanua jeografia ya maeneo ya utalii sambamba na kuongeza
vivutio ili kuongeza idadi ya watalii na mapato.
Amesema
Serikali itajenga makumbusho ya Marais Wastaafu wa Tanzania mjini
Dodoma pamoja kuanzisha makumbusho ya meno ya tembo katika miji ya Dar
es Salaam, Arusha, Iringa na Dodoma.
Sambamba
na hayo amesema Serikali itaanzisha mwezi maalum wa maadhimisho ya
urithi wa Mtanzania ambao utafanyika mwezi Septemba kila mwaka pamoja na
kuendeleza utalii wa mikutano.
Amesema
Serikali pia itaanzisha Mamlaka ya Usimamizi na Uendelezaji wa Fukwe
nchini ili kuimarisha utalii wa fukwe pamoja na kutambua barabara
iliyokuwa ikitumika katika biashara ya utumwa wakati wa ukoloni ili
iweze kutumika kiutalii.
Akizungumzia
migogoro ya mipaka iliyopo baina ya wananchi na maeneo ya hifadhi, Dk.
Kigwangalla alisema Serikali itatatua migogoro hiyo kwa kushirikisha
wananchi sambamba na kuwasaidia kutatua changamoto za msingi ambazo ni
kuimarisha maeneo ya malisho ya mifugo, upatikanaji wa maji kwa ajili ya
wananchi na mifugo, mpango bora wa matumizi ya ardhi na uendelezaji wa
kilimo na ufugaji.
Kwa
upande wake balozi Cooke alisema nchi yake itaendelea kuimarisha
ushirikiano inaoutoa kwa Serikali ya Tanzania katika kudhibiti mtandao
wa uhalifu wa madawa ya kulevya, rushwa na ujangili.
Alisema
kwa sasa watalii zaidi ya 75,000 wa Uingereza hutembelea Tanzania kila
mwaka na wengine wamewekeza katika sekta utalii hapa nchini, hivyo
akaiomba Serikali kurekebisha baadhi ya changamoto chache zilizopo
katika sekta hiyo kwenye mtiririko wa kodi.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na balozi wa
Uingereza hapa nchini, Sarah Cooke ofisini kwake mjini Dodoma jana
ambapo walijadili mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano katika
sekta ya uhifadhi na maendeleo ya utalii.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla.
Balozi wa Uingereza hapa nchini, Sarah Cooke.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiaga na balozi wa
Uingereza hapa nchini, Sarah Cooke ofisini kwake mjini Dodoma jana baada
ya mazungumzo yaliyolenga walijadili mambo mbalimbali ya kuimarisha
ushirikiano katika sekta ya uhifadhi na maendeleo ya utalii.
Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akiagana na msafara wa
balozi wa Uingereza hapa nchini, Sarah Cooke ofisini kwake mjini Dodoma
jana ambapo walijadili mambo mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano katika
sekta ya uhifadhi na maendeleo ya utalii.
Post a Comment