PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MSANII MAARUFU AFRIKA MASHARIKI ALI KIBA AFUNGA NDOA ASUBUHI YA LEO MJINI MOMBASA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
       STAA wa muziki wa  Bongo Fleva nchini, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’, amefunga ndoa na mchumba wake Amina Khalef, leo asub...



Hatimaye Imetimia Alikiba Afunga Ndoa Asubuhi Mjini Mombasa
 STAA wa muziki wa  Bongo Fleva nchini, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’, amefunga ndoa na mchumba wake Amina Khalef, leo asubuhi, Aprili 19, mjini Mombasa nchini Kenya.

Hakika ni furaha, shangwe, nderemo na vifijo kwa maharusi, wanafamilia na mashabiki wa Kiba mara baada ya ndoa hiyo kufungwa katika msikiti wa Ummul Kulthum, mjini Mombasa.

Katika shughuli hiyo ya kihistoria kwa msanii huyo, Kiba ameandamana na mdogo wake, Abdul Kiba na na rafiki yake ambaye ni Gavana wa Mombasa, Hassan Joho ambaye ndiye amesimamia mipango yote ya harusi hiyo nchini humo.

Ilikuwa ni baada Koran kusomwa, na Sheikh Mohammed Kagera akakinyanyua kiganja cha Alikiba na kumuozesha kwa Amina Khalef.

“Mimi Ali Saleh nimekubali kumuoa Amina Khalef kwa mahari tuliyokubaliana na ikitokea sababu ya kuachana tuachane kwa wema,” amesema Kiba wakati akifunga ndoa yake.

Katika shughuli hiyo, Kiba alivaa joho na kilemba, alishika upanga kama desturi ya tamaduni ya zinavyomtaka na baada ya kutoka msikitini waalikwa wamekwenda nyumbani kwa ndugu wa Joho, Abu Joho, Kizingo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top