PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MAJAMBAZI WENYE SILAHA WATEKA KITUO CHA MAFUTA JIJINI ARUSHA NA KUPORA MAMILIONI YA FEDHA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
  Watu wanaosadikiwa kuwa ni Majambazi wapatao wanne wakiwa wamevalia Makoti Meusi na silaha za Moto wamevamia kituo cha Ma...

 



Image result for manjis petrol station arusha
Image result for manjis petrol station arushaImage result for manjis petrol station arusha
Watu wanaosadikiwa kuwa ni Majambazi wapatao wanne wakiwa wamevalia Makoti Meusi na silaha za Moto wamevamia kituo cha Mafuta cha Manjis cha jijini hapa na kufanikiwa kupora kiasi cha sh, milioni mbili zikiwa ni  fedha za Mauzo .

Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa polisi Mkoa wa Arusha Yusufu Ilembo, akiongea ofisini kwake leo,  tukio hilo limetokea Jana April I6, majira ya saa moja na nusu usiku Katika barabara ya Uhuru katikati ya Jiji la Arusha

Amesema kuwa   majambazi hao walifika eneo la tukio wakitembea Kwa mguu na kuwalazimisha wafanyakazi waliokuwepo katika kituo hicho kulala chini huku wakifyatua risasi mbili hewani na kuelekea ndani ya ofisi zinapohifadhiwa fedha.

Anasema majambazi wawili waliingia ndani huku wawili wakibakia nje kudhibiti raia na baadaye wenzao walitoka wakiwa na  na kiasi hicho cha fedha na kufanikiwa kutokomea kusiko julikana wakiwa wanatembea

Hata hivyo uongozi wa kituo hicho umelalamikia hatua ya jeshi la Polisi kuchelewa kufika eneo la tukio na hivyo kuwapa nafasi majambazi hao kupora kiulaini na kuondoka bila kubughudhiwa.

Polisi wa doria wanadaiwa kufika baada ya nusu saa zaidi ,ya muda wa tukio na kukuta majambazi wameshatoweka eneo hilo

Kamanda Ilembo amekiri Polisi kuchelewa kufika akijitetea yakuwa Magari ya doria yalikuwa eneo lingine la Kwa Morombo umbali wa takribani kilometa moja toka eneo la tukio na hivyo kuchukua muda kufika .

Katika tukio hilo hakuna aliyejeruhiwa na Polisi wameanza uchunguzi wa tukio hilo na kwamba hadi sasa hakuna anayeshikiliwa kuhusika na tukio hilo.

Hata hivyo habari tulizozipata leo za Tukio la Uporaji wa fedha Katika kituo cha Mafuta cha Puma (Manjis) lililotekelezwa na Majambazi wapatao wanne ,wenye silaha za moto ,Imefahamika kuwa kiasi cha zaidi ya sh,milioni 20,000 za Mauzo ziliporwa.

Aidha wafanyakazi sita wa kituo hicho wameshikiliwa na polisi na wanahojiwa tangu jana kuhusiana na tukio hilo.

Mwendeshaji wa kituo hicho cha Mafuta,Mehboob Sajan Akiongelea tukio hilo amesema kuwa Kwa wastani wa Mauzo yao Kwa siku ni  zaidi ya Lita 10,000 zenye thamani ya kiasi hicho cha fedha.
"Mauzo yetu Kwa siku ni zaidi ya Lita 10,000 sasa ukijumlisha na Mauzo ya Oil inaweza kuwa zaidi ya sh,milioni 20" Amesema Sajan.

Aidha ameongeza kuwa Polisi inawashikilia wafanyakazi wao sita waliokuwa zamu siku ya tukio lililotokea hapo juzi majira ya saa moja usiku,April 15.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top