Darasa la mafunzo kazini likiendelea kwa wafanyakazi wa Hoteli za Chem chem, katika eneo la hifadhi ya jamii ya wanyamapori ya Burunge, wilayani Babati mkoani Manyara |
Baadhi ya wafanyakazi wa Hoteli za Chem chem, katika eneo la hifadhi ya jamii ya wanyamapori ya Burunge, wilayani Babat wakipatiwa mafunzo ya lugha ya kiingereza ili kukabiliana na changamoto hiyo |
ANDREA NGOBOLE, PMT ARUSHA
Sekta
ya Utalii nchini, inakabiliwa na uhaba wa wafanyakazi wenye sifa hatua
inayochangia, kushindwa kupambana na mataifa mengine katika kuvutia
watalii hivyo serikali na vyuo vinavyotoa elimu ya Utalii, wameombwa kuboresha mitaala ili kwendana na mahitaji katika soko la ajira.
Katibu
Mtendaji wa chama cha waajiri katika nchi za Afrika ya Mashariki(EAEO)
Dk Aggrey Mlimuka, akizungumzia tatizo la uhaba wa wafanyakazi wa sifa
linazikabili nchi zote za afrika ya Mashariki alisema, nusu wa wahitimu wa vyuo vikuu katika nchi hizo, hawana sifa stahiki katika soko la ajira.
Katika
kukabiliana na tatizo hilo,Mwekezaji wa Hoteli za Chem chem, katika
eneo la hifadhi ya jamii ya wanyamapori ya Burunge, wilayani Babati,
ameamua kuanza kuwafunisha wafanyakazi wake 160.
Meneja
wa Chemchem Foundation, Charles Sylivesta alisema, wameamua
kuwafundisha wafanyakazi,kulingana na mahitaji ya idara zao ili
kuwaongezea uwezo wa kufanyakazi hasa kuhudumia watalii.
"wanafundishwa
kiingereza,ubishi, kuandaa Vyumba vya kulala watali na kuongoza watalii
na tuna wataalam wa ndani na nje ya nchi"alisema.
Meneja
wa Chemchem Lodge Kelly Ricklan alisema mafunzo hayo, yatasaidia
wafanyakazi wao ambao wengi wao wanaishi katika eneo la Burunge kupata
uwezo wa kufanyakazi vizuri.
Akizungumza
katika mafunzo hayo, Mwalimu wa lugha katika hoteli hizo,John Macha
alisema, baadhi ya wafanyakazi wamekuwa wakikabiliwa na wakati mgumu
kuwasiliana na watalii.
"kipindi
hiki hatuna wageni wengi, tumeamua kuwafundisha lugha mbali mbali za
kimataifa ili waweze kuwasiliana vyema lakini pia waapewa mafunzo ya
wataalam wengine"alisema
Mmoja
wa wafanyakazi wa hoteli hizo,Happy Mtani alisema mafunzo hayo,
yamekuwa na msaada mkubwa kwao kwani inawasaidia kuoboresha utendaji wa
kazi zao.
Post a Comment