PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: TAASISI YA JAKAYA KIKWETE (JMKF) KUWANUFAISHA WANYONGE WOTE BARANI AFRIKA
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
 Msanii anayechipukia  Goodluck Gozbert akitumbuiza kwa wimbo wake maarufu wa "Hauwezi Kushindana" kwenye hafla...

 Msanii anayechipukia  Goodluck Gozbert akitumbuiza kwa wimbo wake maarufu wa "Hauwezi Kushindana" kwenye hafla ya uzinduzi wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza msanii anayechipukia  Goodluck Gozbert baada ya kutumbuiza kwa wimbo wake maarufu wa "Hauwezi Kushindana" kwenye hafla ya uzinduzi wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
 Mshauri mwelekezi wa JMKF Bi. Aisha Sykes akiwa na mwezeshaji Aidan Eyakuze wakifanya mawasilisho ya mpango mkakati wa tasisi hiyo kwenye hafla ya uzinduzi wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea  kwenye hafla ya uzinduzi wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
 Wageni waalikwa wakimsikiliza Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea  kwenye hafla ya uzinduzi wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018

 Wajumbe wa Baraza la wadhamini wa JMKF wakiwa katika hafla hiyo

 Wageni waalikwa wakimpigia makofi  Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kuongea  kwenye hafla ya uzinduzi wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
 Mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kuhutubia katika hafla ya uzinduzi wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
 Mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiteta jambo na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  katika hafla ya uzinduzi wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2019
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018. wengine meza kuu kutoka kushoto ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo Bw. Omari Issa
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia katika hafla ya uzinduzi wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018. wengine meza kuu kutoka kushoto ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
Sehemu ya mabalozi wa nchi mbalimbali wakiwa  kwenye hafla ya uzinduzi wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018

 Sehemu ya wageni waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia  kwenye hafla ya uzinduzi wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipigiwa makofi baada ya kuhutubia katika hafla ya uzinduzi wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018. wengine meza kuu kutoka kushoto ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
 Mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  baada ya kuzindua rasmi taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
 Sehemu ya wageni waalikwa   kwenye hafla ya uzinduzi wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
Meza kuu ikimsikilia mjumbe wa Baraza la Wadhamini wa taasisi hiyo Bw. William Mahalu akitoa neno la shukrani baada ya  ya uzinduzi wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
 Sehemu ya mabalozi wa nchi mbalimbali wakiwa  kwenye hafla ya uzinduzi wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
 Wajumbe wa Baraza la Wadhamini wa taaisi hiyo - Profesa Rwekaza Mukandala na Balozi Ombeni Sefue - wakiwa  kwenye hafla ya uzinduzi wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
 Wajumbe wa Baraza la Wadhamini wa taaisi hiyo - Bw. Abubakar Bakhressa na Bi.Genevieve Sangudi  - wakiwa  kwenye hafla ya uzinduzi wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018

 Sehemu ya wageni waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia  kwenye hafla ya uzinduzi wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
 Sehemu ya wageni waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia  kwenye hafla ya uzinduzi wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
 Mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan wakimsikiliza  mjumbe wa baraza la wadhamini wa JMKF Genevieve Sangudi  akitoa shukurani baada ya uzinduzi rasmi wa taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
 Mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipeana mikono na  mjumbe wa baraza la wadhamini wa JMKF Genevieve Sangudi  baada ya kushukuru kwa uzinduzi rasmi wa taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
 Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi akipeana mikono na mjumbe wa baraza la wadhamini wa JMKF Genevieve Sangudi  baada ya kushukuru kwa uzinduzi rasmi wa taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
 Sehemu ya wageni waalikwa wakimsikiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akihutubia  kwenye hafla ya uzinduzi wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
 Mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakisalimiana na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama  baada ya kuzindua rasmi taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018

 Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete baada ya uzinduzi rasmi wa taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
 Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Miraji Kikwete baada ya uzinduzi rasmi wa taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
 Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wanafamilia yake baada ya uzinduzi rasmi wa taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
  Mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakiongea jambo na Mbunge wa Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete na Miraji Kikwete  baada ya kuzindua rasmi taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
  Mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Makamu wa Rais wakiondoka ukumbini baada ya kuzindua rasmi taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
  Mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Waziri wa MAmbo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga pamoja na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwlimu katika picha ya pamoja na wajumbe wa baraza la washamini wa taaisi baada ya uzinduzi rasmi wa taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018

 Mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Waziri wa MAmbo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga pamoja na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwlimu katika picha ya pamoja na mabalozi baada ya uzinduzi rasmi wa taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
 Mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Waziri wa MAmbo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga pamoja na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwlimu katika picha ya pamoja na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama  baada ya uzinduzi rasmi wa taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
 Mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Waziri wa MAmbo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga pamoja na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwlimu katika picha ya pamoja na wanafamilia wa Kikwete  baada ya uzinduzi rasmi wa taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
 Mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Waziri wa MAmbo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine Mahiga pamoja na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwlimu katika picha ya pamoja na wake wa viongozi baada ya uzinduzi rasmi wa taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
  Mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea CD toka kwa msanii Goodluck Gozbert  baada ya uzinduzi rasmi wa taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
  Mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan wakielekea kupata chakula cha jioni  baada ya uzinduzi rasmi wa taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
  Mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan wakiongea na mjumbe wa baraza la wadhamini wa JMKF Genevieve Sangudi  baada ya uzinduzi rasmi wa taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
 Mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan wakiwakaribisha mabalozi kwa chakula cha jioni  baada ya uzinduzi rasmi wa taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018

 Wanafamilia wakiwa katika chakula cha jioni  baada ya uzinduzi rasmi wa taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa na  Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais Mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi na Mtendaji Mkuu wa taasisi hiyo Bw. Omari Issa
  Wanafamilia wakiwa katika chakula cha jioni  baada ya uzinduzi rasmi wa taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018

  Wanafamilia wakiwa katika chakula cha jioni  baada ya uzinduzi rasmi wa taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
  Wageni waalikwa wakiwa katika chakula cha jioni  baada ya uzinduzi rasmi wa taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018

 Wake wa viongozi wakiwa katika chakula cha jioni  baada ya uzinduzi rasmi wa taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
  Mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mama Sitti Mwinyi  baada ya uzinduzi rasmi wa taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
   Mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Balozi Ombeni Sefue  baada ya uzinduzi rasmi wa taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
   Mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na mjumbe wa baraza la wadhamini Bw. Abubakar Bakhressa  baada ya uzinduzi rasmi wa taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
   Mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Ofisa ubalozi wa Kuwait nchini Bw. Mohammad Rashidi Alamiri baada ya uzinduzi rasmi wa taasisi ya  Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
 Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa na wake wa viongozi wakiongea na mjumbe wa baraza la wadhamini wa JMKF baada ya hafla ya uzinduzi wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018
Mgeni rasmi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akaigana  na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete  baada ya hafla ya uzinduzi wa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF) katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Ikulu jijini Dar es salaam Jumatano Aprili 11, 2018. Picha na IKULU
*Azungumzia mambo makubwa ambayo aliyafanya kwenye utawala wake ambayo yatakumbukwa 
 *Azindua rasmi Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete Foundation,aahdi Serikali kutoa ushirikiano mkubwa 
 *Alezea Kikwete alivyosababisha awe Rais wa Awamu ya Tano, Kikwete azungumzia malengo ya taasisi 

 Na Said Mwishehe, Globu ya Jamii. 
 RAIS Dk. John Magufuli amesema kwa kazi kubwa ambayo imefanywa na Rais mstaafu Jakaya Kikwete kwenye uongozi wake kuna mambo makubwa ya maendeleo katika nchi yetu huku akitanguliza uzalendo mkubwa Watanzania wanamkumbuka na wataendelea kukumbuka watake wasitake. Pia ametumia nafasi hiyo kutoa shukrani zake za dhati kwa Rais mstaafu Kikwete kwani ndio amesababisha awe Rais wa Serikali ya Awamu ya Tano huku akitumia nafasi hiyo kuahidi kuwa atahakikisha Serikali yake itashirikana na Taasisi ya Jakaya Mrisho Kikwete inayofahamika kwa Jakaya Mrisho Kikwete Foundation (JMKF)ambayo ameizindua rasmi leo Ikulu jijini Dar es Salaam. "Mzee wangu Kikwete naomba niseme kutoka moyoni wakati wa uongozi wako umefanya mambo makubwa ya kuleta maendeleo kwa ajili ya nchi yetu ya Tanzanania.Kuna miradi mikubwa ya maendeleo ambayo ameifanya na imeacha alama ambayo itatufanya watanzania tumkumbuke.Kwa kazi ambayo umeifanya kwa uzalendo mkubwa ndani ya nchi yetu Watanzania tunakukumbuka na tutaendelea kukumbuka watake wasitake,"amesema Rais Dk.Magufuli. Ametaja ipo mifano mingi hai ya mambo ambayo ameyafanya Rais mstaafu Kikwete kwenye Serikali ya Awamu ya nne na baadhi ya miradi hiyo lipo la ujenzi wa bomba la gesi kutoka mkoani Mtwara hadi Dar es Salaam, ujenzi wa miundombinu ya barabara nchi nzima, ujenzi wa miradi ya maji , umeme na kuimarisha sekta muhimu za afya, kilimo na vijana. 
 "Rais mstaafu Kikwete alilitumikia Taifa la Tanzania kwa uadilifu mkubwa. Tabia ya binadamu wamekuwa na kawaida ya kumsifu mtu baada ya kufa na kusema pengo halitazibika wakati si kweli kwani kama ni nafasi ya uongozi inaweza kujazwa wakati huohuo. Kwa Rais mstaafu na mzee wangu Kikwete naomba nikusifu ukiwa hai tena upo mbele yangu unatabasamu. 

"Umefanya kazi kubwa ya kizalendo kwa ajili ya nchi yetu ya Tanzania na unastahili sifa na shukrani kutokana na mchango wao wa kuleta maendeleo kwenye nafasi mbalimbali. 
 "Ulipokuwa Rais wa Tanzania umefanya mambo makubwa zaidi kwa ajili ya nchi yetu. Katika utawala wako umefanikisha ujenzi wa shule za sekondari za kata , ujenzi wa Hospitali ya Mloganzila na miradi mingine mikubwa ambayo umeifanya na sote ni mashahidi kwa yale ambayo umeyafanya,"amesisitiza Rais Dk.Magufuli na kuongeza mbali ya kuwa Rais mzee Kikwete ameshika nafasi mbalimbali za uongozi ndani ya Bara la Afrika na nchi za ulaya na Dunia kwa ujumla na kote huko ametoa mchango mkubwa wa kuleta maendeleo . 
 Rais Magufuli amesema uzalendo wa mzee Kikwete kwa nchi yake umemfanya hata baada ya kustaafu kuamua kuanzisha taasisi ambayo leo amezindua rasmi na vipaumbele vya taasisi hiyo havina tofauti na vile ambavyo anavitekeleza kwenye Serikali yake , hivyo ameahidi kumpa ushirikiano mkubwa kufanikisha malengo hayo na kuomba wadau wengine wakiwamo mabalozi nao kuunga mkono kazi za taasisi hiyo. 
 "Mzee Kikwete ameiga mfano wa watangulizi wake kuanzia Mwalim Nyerere, Mzee Mwinyi na mzee Mkapa ambao nao baada ya kustaafu kuongoza nchi waliamua kuendelea kutoa mchango wao wa kulitumikia taifa na hivyo kitendo cha Rais mstaafu Kikwete kuanzisha taasisi hiyo imeonesha uzalendo na utayari wake wa kuendelea kutoa mchango wake kwa nchi yake na Bara la Afrika kwa ujumla kwani taasisi hiyo itatoa huduma zake ndani na nje ya nchi yetu,"amesema. 

 AZUNGUMZIA VIPAUMBELE VYA TAASISI 
 Rais Dk.Magufuli ameeleza namna ambavyo amefurahishwa na vipaumbele vyake katika kuwatumikia Watanzania na Bara la Afrika kwa ujumla.Amefafanua kuna vipaumbele vinne na kipaumbele cha kwanza ni eneo la afya na Watanzania wanafahamu umuhimu wa eneo la afya kwani ili nchi iwe na maendeleo lazima watu wake wawe na afya njema. 
 Amesema Serikali yake imeendelea na jitihada za kuhakikisha inapunguza vifo kwa mama mjazito na watoto chini ya miaka mitano na kufafanua kuwa Rais mstaafu Kikwete akiwa madarakani alifanikiwa kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi na watoto wenye umri chini ya miaka mitano. 

"Nimefurahi kuona suala la afya limepewa kipaumbele kwenye taasisi hii mpya ambayo naizindua leo hii. Nami kwenye Serikali nimeendelea kuboresha vituo vya afya na sasa tunaendelea na upanuzi wa vituo vya afya 170 ambapo lengo viwe vinafanya upasuaji kwa mama wajawazito ili kuokoa maisha,"amesema Rais Dk Magufuli na kuongeza wanaendelea na kutoa chanjo kwa watoto chini ya miaka mitano na lengo ni kupunguza vifo,"amesema. 
 Amesema kipaumbele cha pili ni vijana na kueleza kuwa kuna changamoto nyingi katika kundi hilo ambalo linahitaji kusaidiwa na taasisi ya Rais mstaafu Kikwete imeamua kuelekeza nguvu zake wakati kipaumbele cha tatu ni sekta ya kilimo na kwa Tanzania sehemu kubwa ya watu wake wamejikita kwenye sekta hiyo.
Kipaumbele cha nne ni utawala bora na amani na kufafanua nalo ni eneo muhimu na kueleza vipaumbele vyote hivyo navyo ndivyo vipaumbele vyake na hata kwa nchi nyingine za Afrika. "Taasisi hii imeahidi kushirikiana na Serikali na si kushindana.Hivyo tutahakikisha tunashirikiana nayo kwa karibu na nieleze tu sitakuwa tayari kushirikiana na taasisi yenye lengo la kuvuruga amani ya nchi na ninakushukuru mzee Kikwete umeeleza wazi namna ambavyo utashirikiana nasi,"amesisitiza. 
 Rais Magufuli ameeleza namna ambavyo anamshukuru Rais mstaafu Kikwete na kufafanua hata yeye kuwa Rais imetokana na yeye na huo ndio ukweli, hivyo popote atakapomuana ataendelea kumshukuru. 

Pia amewashukuru viongozi wengine wa ngazi mbalimbali na anafurahia kuona wapo marais wastaafu wamemzunguka na kumpa ushauri na maelekezo yanayomsaidia kutekeleza majukumu yake. 

 KIKWETE AMSHUKURU DK MAGULI, AZUNGUMZIA TAASISI YAKE 
 Kwa upande wake Rais Mstaafu Kikwete amesema kuwa anamshukuru Rais Magufuli kwa kukubali kuzindua taasisi hiyo na kuipa heshima ya hali ya juu na kutumia nafasi hiyo kuahidi kuwa lengo la kuanzishwa kwa taasisi hiyo ni kufanya kazi katika maeneo ambayo wameamua kuanza nayo zaidi kama sehemu ya kutoa mchango wao katika kushirikiana na Serikali kutekeleza majukumu yake. 
 Amefafanua wakati anakaelekea kustaafu , alianza kufikiria akiwa na wasaidizi wake nini afanye baada ya kustaafu na hivyo walikubaliana mambo mawili, moja kuanzisha taasisi hiyo na mbili kuandika kitabu ambacho nacho atakifanikisha. 
 Amelezea maeneo ambayo wamekubaliana na bodi ya wadhamini wa taasisi hiyo ya kuanza nayo na kufafanua wanatambua yapo maeneo mengi lakini wameanza na mambo manne likiwemo eneo la afya ya mama mjazito na mtoto."Ni falsafa na sera ya msingi kuwa tutafanya kazi kwa karibu na Serikali na hakuna sababu ya kusigana na Serikali na hatutakubali kushawishiwa na mtu yoyote." 
 Ameongeza Serikali ndio washirika namba moja na kueleza kuwa hivyo wao wanachokifanya ni kuendelea kusaidia kazi inayofanywa na Rais Dk.Magufuli na nchi nyingine za Afrika.
Shabaha yao ni kwamba pale ambao wengine wapo wao hawatakwenda na hata wakienda basi ni kuongeza nguvu na kubwa zaidi hakuna wanayeshindana naye. 
 "Nakushukuru Rais kwa moyo wako wa upendo kwangu na Watanzania kwa ujumla na kwamba kazi kubwa ya kuleta maendeleo ambayo unaifanya sote tunaiona.Natambua kunachangamoto nyingi ambazo unakabiliana nazo lakini tutaendelea kukuombea kwa Mungu ili utekeleze vema majukumu yako,"amesema Rais mstaafu Kikwete.

About Author

Advertisement

Post a Comment

Top