picha ikionyesha mtoto Abdul
Hussein mwenye Umri wa Miaka 7 mkazi wa daraja Mbili jijini Arusha
anayesumbuliwa na maradhi ya Mtindio wa Ubongo pamoja na ulemavu wa
viungo anaishi Kwa mateso makubwa kwani tangu azaliwe hajawahi kuamka
,kuona wala kusikia akiwa anapewa maziwa na mama yake Ashura Hussen
,mama huyu anaomba msaada wa kifedha kwa wananchi ,viongozi wa dini
,wabunge pamoja na Rais ili apate fedha za kumpeleka mtoto wake nje ya
nchi kwa ajili ya matibabu (picha na Woinde Shizza,Arusha)
baadhi
ya waandishi wa habari wakikabidhi vitu ambavyo wamechanga kwa ajili ya
kumsaidia mama huyo ambaye ameacha kazi kutokana na kumlea mtoto huyo
tangu amzae
Theodora
Mrema mwandishi wa Star Tv mkoa wa Arusha akikabidhi sabuni ikiwa ni moja ya michango
iliyotolewa na waandishi wa habari wa mkoa wa Arusha
Geofrey
Steven mwandishi wa Radio 5 akiwa anakabidi baadhi ya nguo zilizotolewa
na waandishi wa habari waliomtembelea mtoto huyo
hawa
ni baadhi ya waandishi wa habari wa mkoa wa Arusha waliojitolea
kumtembelea mtoto Abdul anaesumbuliwa na ugonjwa wa mtindio wa ubongo
Na Woinde Shizza,Arusha
Mtoto
Abdul Hussein mwenye Umri wa Miaka 7 mkazi wa daraja Mbili jijini
Arusha anayesumbuliwa na maradhi ya Mtindio wa Ubongo pamoja na ulemavu
wa viongo anaishi Kwa mateso makubwa kwani tangu azaliwe hajawahi
kuamka ,kuona wala kusikia.
Mama
mzazi wa mtoto Huyo Ashura Hussein Amesema kuwa mtoto wake huyo amekuwa
na matatizo tangu azaliwe na aligundulika kuwa na tatizo LA mtindio wa
Ubongo akiwa na umri wa miaka miwili
Mtoto
wangu Siku nilipojifunga katika hospitali ya Temeke,Dar Siku ya kwanza
hakuweza kulia ama kunyonya kama ilivyo kwa watoto wengine.
"Madaktari
walimwekea mpira wa maziwa ,baadae baada ya mwaka alianza kunyonya na
ilipofika mwaka mmoja na nusu alikuwa akining'ata anapokuwa akinyonya
ndipo madaktari wakaniambia ni mwachishe kumnyonyesha ndipo
nikamwachisha na akaanza kutumia mpira tangu hapo "Amesema mama Mzazi
Aidha
Alisema kuwa alianza kumpa chakula na mpira na alipofikisha umri wa
miaka miwili alikumbwa na tatizo kutapika kila anapokula chakula tatizo
lililoendelea hadi sasa ambapo kwa sasa anapewa chakula kupitia
mrija Kwa kutumia bomba la sindano lakini pindi anapokula akikaa baada
ya muda mchache amekuwa akirudisha chakula chote kwa kutapika
"kutokana
na matatizo haya kwakweli mimi nilikuwa nesi imenibidi niache sifanyi
kazi yoyote nakaa tu hapa nyumbani kwani siwezi hata kwenda kuajiriwa
maana siwezi kwenda na mtoto hivyo naishi maisha ya shida sana kusema
kweli jamani angalau hata ningekuwa hata na kaofisi ka kuniingizia
riziki "aliseama Ashura mama mzazi wa Abudul
Mama
Huyo amewaomba wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali wabunge
na Rais John Magufuli kuweza kumsaidia ili apate fedha Kwa ajili ya
kumpatia matibabu nje ya nchi mtoto huyu .
Post a Comment