Baadhi ya silaha alizokamatwa nazo mtuhumiwa wa ujangili |
mtuhumiwa wa ujangili akiwa amewekwa chini ya ulinzi baada ya kukamatwa |
Msako wa kukabiliana na majangili wa misitu na wanyamapori , katika eneo la pori la akiba la Ugalla, umefanikiwa kumkamata mtuhumiwa wa ujangili,Moshi Bakari akiwa na mbao aina ya mninga na bunduki yenye risasi 39.
Akizungumza mapema jana, Meneja msaidizi wa kitalu
cha uwindaji cha Ugalla kinachomilikiwa na kampuni ya uwindaji ya
Tanzania Game Trackers Safaris(TGTS) yenye makao makuu yake jijini
Arusha, Dago Ally alisema mtuhumiwa huyo amekamatwa juzi.
Ally alisema, katika operesheni hiyo ambayo inashirikisha
askari wa pori la akiba ya Ugalla na vyombo vya usalama mtuhumiwa huyo,
licha ya kukutwa na Bunduki hiyo aina ya Gobole pia amekamatwa na
Msumemo, Kisu na shoka.
"hawa watuhumiwa wa ujangili walikuwa watatu na wawili walifanikiwa kukimbia"alisema
Akizungumzia matukio ya ujangili msimamzi idara ya ulinzi
wa katika kitalu hicho wa taasisi ya Friedkin Conservation Fund, Suphian
Kisseko alisema tukio hilo ni la pili ndani ya miezi miwili kukamata
majangili.
Alisema machi 12 mwaka huu, walifanikiwa pia kukamata,
watuhumiwa wawili wa ujangili Shindwa Shugela(47) na Amka Lalaa(46)
ndani ya pori la akiba wakiwa na bunduki aina ya Gobole , baruti
gramu85,Goroli 48 na fataki 17.
Kisseko pia alisema, waliwakamata na meno mawili ya ngili,meno mawili ya kiboko na nyama ya Ngili na Dikidiki.
"Hivi sasa kutokana na ushirikiano katika vita vya
kupambana na ujangili tumejipanga kuhakikisha hakuna jangili ambaye
anaweza kuingia katika pori la akiba la ugalla na kutoka salama"alisema
Alisema watuhumiwa wote hao, baada ya kukamatwa katika
operesheni ambazo zinaendelea, wamekuwa wakikabidhiwa katika vyombo vya
dola kwa hatua zaidi za kisheria.
Post a Comment