Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Msimamizi
wa Makampuni ya Albawardi, Fouad Mustafa ya Umoja wa Falme za Kirabu
ofisini kwake Jijini Dodoma jana ambapo walijadili uwekezaji wa
kuimarisha sekta ya utalii na uhifadhi nchini. Umoja huo umeahidi kutoa
ushirikiano wa ujenzi wa barabara inayounganisha Hifadhi ya Ngorongoro
na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
.............................. .............................. .............
WAZIRI
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla ameonana na kufanya
mazungumzo na Balozi wa Saudi Arabia na Kuwait pamoja na Msimamizi wa
Jumuiya ya Makampuni ya Albawardi inayoendesha hoteli mbalimbali za
kitalii nchini ikiwemo Hyatt Regency na Four Season Serengeti ofisini
kwake Jijini Dodoma jana.
Mazungumzo
hayo yaliyolenga kujadili mambo mbalimbali ya kuimarisha sekta ya
uhifadhi na utalii kwa maslahi ya nchi hizo tatu. Mabalozi hao ni Bandar
Abdulla wa Saudi Arabia, Mohammad Rashed Alamiri wa Kuwait na Fouad
Mustafa Msimamizi wa Makampuni ya Albawardi ya Umoja wa Falme za Kirabu
kwa upande wa Tanzania na Afrika ya Mashariki.
Dk.
Kigwangalla aliwaomba mabalozi hao kupitia jumuiya zao za uwekezaji
kuwekeza katika miundombinu ya hoteli za kitalii Jijini Dodoma na kwenye
Mapori ya Akiba katika Sakiti ya Kaskazini, Kusini na Magharibi hususan
Pori la Akiba la Burigi.
Naye
Msimamizi wa Jumuiya ya Makampuni ya Albawardi, kwa upande wa Tanzania
na Afrika ya Mashariki, Fouad Mustafa alisema jumuiya hiyo ipo tayari
kutoa ushirikiano kwa Serikali ya Tanzania katika ujenzi wa miundombinu
ya barabara inayounganisha Hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti.
Alisema
mbali na uwekezaji uliopo hivi sasa jumuiya hiyo inajenga hoteli
nyingine za kitalii tatu katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Hifadhi
ya Ngorongoro na katikati ya Jijini la Arusha ambapo ameiomba Serikali
kuzifungua kupitia viongozi wake wa juu pale ujenzi wake utakapokamilika
hususan Mhe. Rais.Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Msimamizi
wa Makampuni ya Albawardi, Fouad Mustafa ya Umoja wa Falme za Kirabu
ofisini kwake Jijini Dodoma jana ambapo walijadili uwekezaji wa
kuimarisha sekta ya utalii na uhifadhi nchini. Umoja huo umeahidi kutoa
ushirikiano wa ujenzi wa barabara inayounganisha Hifadhi ya Ngorongoro
na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.Waziri
wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza na Balozi wa
Kuwait hapa nchini, Mohammad Rashed Alamiri (kushoto) ofisini kwake
Jijini Dodoma jana ambapo walijadili namna ya kuimarisha sekta ya utalii
na uhifadhi nchini. Wa pili kulia ni Msimamizi wa Makampuni ya
Albawardi, Fouad Mustafa ya Umoja wa Falme za Kirabu ambao wameahidi
kutoa ushirikiano wa ujenzi wa barabara inayounganisha Hifadhi ya
Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.Mazungumzo yakiwa yanaendelea.Waziri Kigwangalla akizungumza katika kikao hicho.Waziri Kigwangalla akiagana na msafara huo.
Post a Comment