Baadhi ya Wafanyakazi na Viongozi wa Kiwanda cha Maziwa cha
The Grande Demam wakihakiki ufungashaji wa bidhaa za maziwa zinazozalishwa
kiwandani hapo.Picha na Ferdinand Shayo
|
Baadhi ya Wafanyakazi na Viongozi wa Kiwanda cha Maziwa cha
The Grande Demam wakihakiki ufungashaji wa bidhaa za maziwa zinazozalishwa
kiwandani hapo.Picha na Ferdinand Shayo
|
Baadhi ya Viongozi wa kiwanda cha maziwa cha The Grande Demam wakinywa maziwa
yanayozalishwa na kiwanda hicho
|
Uongozi wa kiwanda cha maziwa cha The Grande Demam
|
Wilaya ya
Meru ni moja kati ya Wilaya maarufu zinazoongoza kwa uzalishaji mkubwa wa
maziwa mkoani Arusha,maziwa ambayo huuzwa maeneo ya miji ikiwemo viunga vya
Jiji la Arusha na nje ya jiji hilo.
Licha ya
uzalishaji huo wa maziwa bado wafugaji hao wanakabiliwa na changamoto ya
ukosefu wa masoko ya uhakika ya kununua maziwa hayo hivyo kupelekea maziwa
wanayoyazalisha kuharibika baada ya kukaa muda bila kununuliwa.
Kufuatia
Changamoto hiyo Moja kati Daktari wa Mifugo Dokta Deo aliona
changamoto hiyo kama fursa ya uwekezaji kwani malighafi ya maziwa inapatikana
kwa wingi ,kwa kuwa wafugaji walikua wakiyamwaga maziwa yao yaliyokua yakiharibika
kwa kukosa soko la uhakika na hawakua na
namna yoyote ya kuongeza thamani maziwa hayo ili yaweze kukaa kwa muda bila
kuharibika.
Dokta Deo
aliacha kazi ya kuajiriwa mwaka 2001 na kuamua kufuga ng`ombe 1 baadae wawili ambao walikua wakitoa lita 40 kila siku huku yeye na familia yake
wakitumia lita 1 hivyo maziwa mengine kuharibika baada ya kukaa kwa muda.
Suala hili
lilimfikirisha sana Dokta Deo ambaye alimtafuta mtaalamu kutoka nchini
Kenya atakayemfundisha jinsi ya kuongeza
thamani maziwa yake ,kuyafungasha na kuyauza .Mtaalamu huyo alimfundisha ndipo
akaianza kazi ya kuongeza thamani maziwa hayo nyumbani kwake.
Baada ya
muda majirani zake wafugaji walianza kuvutiwa na jinsi anavyoongeza thamani
maziwa yake na walimletea maziwa ili ayaongeze thamani ndipo alipoanza kununua
maziwa na kuongeza thamani takribani lita 100,150 mpaka 200 kwa siku.
Baada ya
hapo akafungua kiwanda kidogo ambacho kilikua na uwezo wa kusindika lita 200 kwa siku huku wafugaji wakileta maziwa mengi zaidi
ndipo alipoongeza uzalishaji na kwa sasa anazalisha lita 2000 kwa siku.
Kutokana na
ongezeko hilo lauzalishaji kwa sasa Dokta Deo pamoja na Wakurugenzi wenzake wa
kiwanda hicho cha The Grande Demam wameongeza wigo na kununua maziwa zaidi kwa
wafugaji ambao walikua wakiteseka kupata masoko na wakati mwingine kumwaga
maziwa yao yanayoharibika kwa kukaa muda mrefu bila kununuliwa.
Kiwanda
hicho kinanunua maziwa bora kutoka kwa wafugaji na kuyaongezea thamani ikiwa ni
pamoja na kuyafungasha vyema.
“Maziwa ambayo hayajaongezwa thamani
hukaa kwa muda wa masaa 13 lakini maziwa yaliyoongezwa thamani yanaweza kukaa
hadi mwezi mmoja jambo ambalo linaleta unafuu hasa kwa kipindi kifupi kabla
hayajafika sokoni”
Alisema Dokta Deo
Dokta Deo
anaeleza kuwa maziwa yaliyosindwa ni maziwa mazuri kwa afya ya binadamu yamekua
yameondolewa bacteria hatarishi na kuongezewa bacteria rafiki kwa afya.
Mtu
anayetumia Maziwa ambayo hayajasindikwa anakua yuko hatarini kupata magonjwa
mbalimbali ikiwemo Tb,Typhoid na Brusela.
Pia maziwa
yaliyosindikwa kiwandani yanasaidia kupunguza uwezekano wa kupata magonjwa
yanayoweza kuambukizwa kutoka wanyama kwenda kwa binadamu.
Mkurugenzi
wa kiwanda hicho Dokta Deo amesema kuwa maziwa ni bidhaa yenye faida kubwa sana
katika mwili wa binadamu ikiwemo virutubisho aina ya Protini,Madini,Fat pamoja
na wanga.
Dokta Deo
anashauri unywaji wa maziwa uhamasishwe kwa wingi katika jamii ili kuwa na
jamii yenye afya bora inayoweza kushiriki katika shughuli za uzalishaji.
Anaeleza
kutokana na ubora wa maziwa yanayozalishwa na kiwanda hicho wateja wamekua
wakiyafurahia hivyo wanafirikiria kuongeza uzalishaji na kuboresha zaidi ili
kuwafikia wateja wengi zaidi.
Tuna mpango
wa kuzalisha mpaka lita laki moja kwa siku ,uzalishaji huu utaleta tija kwa
kiwanda pamoja wafugaji ambao tumekua tukinunua maziwa kwao tutanunua maziwa
mengi zaidi hivyo kukuza kipato cha wafugaji waweze kunufaika na shughuli zao
za ufugaji” Alisema Dokta Deo
Ni vyema
Watanzania wakajifunza kunywa maziwa
haya bora yanayozalishwa nchini badala ya kunywa maziwa kutoka nje kwani
kwa kufanya hivyo utakua unainua uchumi wa nje.
Biashara
hiyo ya maziwa imesaidia vijana wengi
waliojiriwa na kiwanda hicho katika sekta ya uzalishaji na usambazaji
jambo ambalo linaonyesha mnyororo wa wanufaika wa kiwanda hicho unavyoongezeka.
Kwa
sasa bidhaa za maziwa,Yogat na Siagi za
The Grande Demam imefika katika mikoa ya Dar es Salaam ,Manyara ,Tanga na
Morogoro.
Mshauri
wa Masuala ya Biashara katika Kiwanda
Peter Ojukwu hicho amesema kuwa kiwanda
hicho kinaweza kuwanufaisha watu zaidi ya 4500 kutokana na mzunguko wa
uzalishaji mpaka kumfikia mlaji.
Anaeleza
kuwa licha ya kiwanda hicho kujikita na uzalishaji wa maziwa bado kinatoa
huduma za ushauri wa ufugaji bora,matibabu ya mifugo pamoja na madawa ili
waweze kufanya ufugaji wenye tija.
Pia
anashauri serikali na taasisi binafsi kuunga mkono juhudi za Wawekezaji
wanaowekeza kwenye viwanda ikiwamo kiwanda cha maziwa kwani kinagusa maisha ya
watu wengi moja kwa moja.
“Kama
unavyojua katika maziwa hakuna kinachosalia unatoa
maziwa,siagi,yogati,samli,mtin di hivyo
hakuna kinachotupwa kila kitu kina thamani kubwa” alisema Mshauri huyo
Nassari na
ni moja kati ya Wafugaji ambao maziwa yao yananunuliwa na kiwanda hicho
wamesema kuwa tangu kuanzishwa kwa kiwanda hicho wamekua wakipata soko la
uhakika la maziwa yao hivyo kuondokana na tatizo la maziwa kuharibika kwa kukosa soko.
Anaeleza
kuwa uwepo wa kiwanda hicho umewasaidia wafugaji wengi ambao walikua hawana pa
kuyapeleka maziwa yao lakini kwa sasa wanafika katika kiwanda hicho na
kuyapeleka maziwa yao.
Post a Comment