Baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria wakifuatilia kikao cha kujadili Makadirio ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka 2018/2019 kilichofanyika Mjini Dodoma. |
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria Mhe.Amina Mollel akiuliza swali wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika Machi 27, 2018. |
Mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Katiba na Sheria Mhe.Saed Kubenea akiuliza swali wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichofanyika Machi 27, 2018 |
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa WCF Bw.Anselim Peter akiwasilisha mada kuhusu Utekelezaji wa sheria ya fidia kwa wafanyakazi kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria Machi 27, 2018. |
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Ajira na Vijana), Mhe. Antony Mavunde akizungumza jambo wakati wa kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kilichofanyika mjini Dodoma. |
(PICHA
ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU – DODOMA)
Na
MWANDISHI WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge, Kazi,Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista
Mhagama ameeleza kuwa uwepo wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni suala muhimu
kuzingatia faida nyingi zitokanazo na mfuko huo tofauti na ilipokuwa awali.
Ameyasema hayo leo mjini
Dodoma wakati wa Uwasilishaji wa Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya
Waziri Mkuu kwa mwaka 2017/2018 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2018/2019
kwa mafungu 25 na 37 kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria.
Waziri Mhagama alieleza kwamba,
miongoni mwa faida za uwepo wa mfuko huo ni pamoja na wafanyakazi kuwa na
maisha bora kutokana na muendelezo wa kipato baada ya kupata ajali au kupoteza
uwezo wa kufanya kazi, mazingira bora na yenye uhakika kazini na waajiri kupata
unafuu wa kulipa gharama mbalimbali endapo mfanyakazi atapata janga kazini kwa
sasa mzigo huu unabebwa na mfuko na kuwa na ongezeko la tija kazini kutokana na
wafanyakazi kufanya kazi kwa ari pamoja na kuwepo kwa wingi kazini.
“Hakika mfuko huu ni mkombozi
mkubwa kwa wafanyakazi na waajiri wote kwa kuzingatia umekuja wakati mwafaka na
umeongeza tija kwa kuwa malengo ya mfuko yanapelekea maisha bora kwa wafanyakazi
na kuleta tija kuzingatia umuhimu wake”.Alisema Mhagama
Pamoja na hayo Waziri
Mhagama aliwapongeza WCF kwa hatua nzuri ya kuanzisha mfuko huo wenye malengo
chanya yatayosaidia kuongeza na kuendeleza azma ya Serikali ya kuwa na Uchumi
wa Viwanda kwa kuwa wafanyakazi watakuwa na mazingira mazuri ya uzalishaji na
ukuzaji wa uchumi wa nchi.
“Kipekee niwapongeze WCF kwa
kuwa na mfuko huu, tunapaswa kuhakikisha unakuwa endelevu na wa mfano kwani unasaidia kuleta
chachu katika ukuaji wa uchumi na kuisaidia Serikali kufikia azma yake ya kuwa
na Uchumi wa Viwanda”.Alisisitiza Mhagama
Naye Mkurugenzi wa
Uendeshaji wa WCF Bw.Anselim Peter alieleza kuwa, mfuko unamajukumu mengi yenye
malengo chanya ikiwemo kusaidia kubuni, kukuza na kuendeleza mbinu za kupunguza
ajali katika maeneo ya kazi.
“Miongoni mwa majukumu ya
mfuko huu, haikuwa kulipa fidia pekee bali kuwa na mbinu mbalimbali za kibunifu
za kupunguza au kumaliza kabisa ajali katika maeneo ya kazi”.Alisisitiza
Anselim.
Aliongeza kuw, kufanikisha
hayo yote,michango ya wabunge ni muhimu katika kutoa uelewa sahihi wa madhumuni
na uendeshwaji wa mfuko huo.
Kwa upande wake mmoja wa
wajumbe wa Kamati ya Katiba na Sheria Mhe.Saed Kubenea (Mb) alipongeza kazi
nzuri inayofanywa na mfuko na kuwaomba kuwa pamoja na mfuko kujali wafanyakazi
wawapo kazini ni vyema pia kuendelea kuhamasisha zaidi kwa kutoa elimu juu ya
mfuko ili umma wa Watanzania kuelewa faida za mfuko huo.
AWALI
Workers Compensation
Fund (WCF) ni Mfuko
wa Fidia kwa Wafanyakazi wa Sekta ya Umma na Binafsi uliochini ya Ofisi ya
Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu na umeundwa kwa mujibu wa kifungu
cha 5 cha sheria ya Bunge ya Fidia kwa wafanyakazi namba 20 ya mwaka 2008
ukiwa na wajibu wa kutoa Mafao ya Fidia kwa mfanyakazi apatwapo na madhara mahala pa kazi.
Post a Comment