Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo, Dk Harrison Mwakyembe leo Jumanne Machi 27, 2018 amekutana na
mwanamuziki Nassib Abdul maarufu Diamond Platnumz, jijini Dar es Salaam
Tarifa iliyotolewa leo na Kaimu Mkuu wa
Kitengo cha Mawasiliano serikalini, Lorietha Laurence imesema lengo la kukutana
kwa wawili hao ni kurejesha maelewano kwenye tasnia ya muziki kufuatia
hatua zinazochukuliwa na wizara hiyo kufungia baadhi ya nyimbo, zikiwemo mbili
za mwanamuziki huyo
Imeeleza kuwa katika kikao hicho
kilichofanyika ofisi za wizara hiyo na kuchukua zaidi ya saa tatu,
kilihudhuriwa na naibu waziri wa wizara hiyo, Juliana Shonza, Katibu
Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Godfrey Mwingereza
Wengine ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu
Tanzania, Joyce Fisoo huku Diamond akifuata na mameneja wake watatu, Sallam
Sharaff, Hamis Taletale na Said Fela
Taarifa hiyo inaeleza mazungumzo hayo,
Diamond alimhakikishia Dk Mwakyembe kushirikiana kwa karibu na Shonza na
uongozi mzima wa wizara katika kusimamia maadili ya kazi za sanaa na kuwa mfano
bora wa wasanii nchini katika kulinda utamaduni wa Tanzania
Kwa upande wake Dk Mwakyembe amesisitiza
kuwa Serikali haina ugomvi wowote na wasanii nchini bali ina tatizo na
mmomonyoko wa maadili, kwamba kila msanii ana wajibu kulinda maadili ambayo ni
sehemu ya utamaduni wa nchi
“Mwakyembe alikumbushia kauli ya Mwalimu
Julius Nyerere baada ya uhuru kwamba Taifa lisilo na utamaduni wake ni sawa na
Taifa mfu na Watanzania kamwe tusigeuke Taifa mfu,” inaeleza taarifa hiyo
ikimnukuu Dk Mwakyembe
Waziri huyo ameagiza watendaji wa wizara na
taasisi zake ikiwemo Basata, Bodi ya filamu na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
(TCRA), kukutana na makundi ya wasanii wa muziki kwa lengo la
kuelimishana kuhusu taratibu za kuwasiliana na mamlaka husika za sanaa
"Maamuzi ya kuzifungia baadhi ya nyimbo
yanayafanywa kwa mujibu wa sheria na si kwa utashi binafsi wa kiongozi wa
wizara. Hivyo basi ieleweke kwamba hatua zilizochukuliwa na Shonza hivi karibuni
zilikuwa za wizara kwa mujibu wa sheria za nchi,” amesema Dk Mwakyembe
Kwa upande wake Shonza amesisitiza umuhimu
wa wasanii kufuata utaratibu kwa kuwasilisha kazi zao mapema kwenye mamlaka
husika iii kuepusha matatizo baadaye
Lorietha Laurence Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo. 27/03/2018.
Post a Comment