Na Rhoda Ezekiel
Watu saba wamefariki dunia katika ajali ya gari aina ya Scania katika Mlima wa Kasagamba kijiji cha Mkongoro barabara ya kutoka Manyovu wilaya ya Kigoma Vijijini kuelekea mkoani Kigoma.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma
Maltini Otieno amesema ajali hiyo imetokea leo Machi 21,2018 majira ya
saa tatu asubuhi.
Amesema gari aina ya Scania lori yenye
namba T741AAB ilianguka na kusababisha vifo vya watu saba akiwemo
dereva wa gari hiyo aliyefahamika kwa jina la Siri Hamis (43) mwenyeji
wa Singida pamoja na utingo wake aliyefahamika kwa jina la Ramadhani
Saidi (23) mkazi wa Manyoni.
Kamanda Otieno amesema katika gari hiyo
walikuwa wamebeba mizigo na watu wanne mmoja mwanamke na wa tatu wanaume
ambapo wote walifariki na majina yao hayakufahamika.
Aidha amesema ajali hiyo pia
imesababisha kifo cha mwanafunzi aliyefahamika kwa jina la Eliakimu
Samsoni (15 )aliyekuwa akitembea kwa miguu kuelekea shuleni na gari hilo
kumgonga akiwa anatembea.
Amesema chanzo cha ajari hiyo ni dereva
kushindwa kuimudu gari kwenye mteremko mkali na kusababisha gari hiyo
kutelemka kwa mwendo mkali na kumshinda dereva huyo na kusababisha vifo
hivyo.
Kamanda Otieno amewaomba
madereva kuzingatia sheria za barabarani na kuhakikisha gari za mizigo
hazibebi abiria ili kunusuru vifo vitokanavyo na ajali na kuhakikisha
wanazingatia alama za barabarani.
Mabaki ya lori baada ya ajali - Picha na Rhoda Ezekiel - Malunde1 blog
Post a Comment