WAZIRI
wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amekamata meli ya uvuvi mali ya
Kampuni ya Buah Naga 1 ya nchini Malaysia na kuitoza faini ya Dola za
kimarekani 350,000 sawa na Sh.milioni 770 kwa kosa la kukutwa na mapezi
ya samaki aina ya papa yenye uzito wa kilo 90 bila miili yake.
Ambapo
hiyo ni kinyume cha Kanuni ya 66 ya kanuni za Mamlaka ya Uvuvi wa
Bahari Kuu pamoja na kifungu cha18 (2) cha Sheria ya Mamlaka ya Uvuvi wa
Bahari Kuu ya mwaka 1998 na marekebisho yake ya mwaka 2007.
Meli
hiyo ilikamatwa Januari 26 mwaka huu baada ya kufanyika ukaguzi
uliosimamiwa na kikosi maalum cha kupambana na kudhibiti uvuvi haramu na
utoroshaji wa samaki na mazao yake wakati ikifanya shughuli za uvuvi
katika ukanda wa Bahari Kuu kati ya Mkoa wa Lindi na Mtwara.Pamoja na
kukutwa na mapezi hayo ya papa, meli hiyo ilikutwa pia na bastola aina
ya Bereta ikiwa na risasi 10 bila ya kuwa na nyaraka za umiliki wake.
Akizungumza
mjini Mtwara ambako meli hiyo ndiko inakoshikiliwa na Serikali Waziri
Mpina ameagiza fedha hizo zilipwe ndani ya siku saba huku akitoa onyo
kali kwa wamiliki wa meli waliopewa leseni za uvuvi wa Bahari kuu
kufuata masharti ya vibali vyao na katika zama hizi za utawala wa Rais,
Dk.John Magufuli watachukuliwa hatua kali zaidi.
"Enzi
za Serikali ya Awamu Tano ya Rais Magufuli mtakaguliwa na kupekuliwa
kuliko wakati wowote, hivyo ni vizuri mkatii sheria za nchi kwa mujibu
wa leseni zenu,"amesema Mpina huku akisilizwa na Kapteni wa meli hiyo
Han Ming Chuan raia wa Taiwan.
Mpina
amesema meli hizo zimekuwa zikitumika pia kufadhili biashara nyingine
haramu ikiwemo kusafirisha dawa za kulevya ,usafirishaji haramu wa
binadamu na biashara ya silaha.Pia zinatumika kutorosha nyara za
Serikali ikiwemo meno ya tembo, samaki na madini.
Aidha
Waziri Mpina amesema kitendo cha wamiliki wa meli hiyo kuwakata samaki
hao mapezi na kisha kutupa miili yao baharini kimeleta athari kubwa kwa
Taifa kwani samaki hao wangeweza kutumika kwa matumizi mengine ya
binadamu na kuchochea uchumi wa nchi.
Hivyo,
ameridhia faini hiyo iliyotozwa na Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu ya
Sh.milioni 770 na kuagiza kilo 90 za mapezi ya samaki na samaki
wasioruhusiwa wataifishwe na kugawiwa kwa wananchi wa maeneo jirani ya
Manispaa ya Mtwara. "Siku nyingine Serikali ikikamata meli iliyofanya
makosa ya aina hiyo itataifishwa pamoja na vitu vyote vitakavyokuwemo
kwa mujibu wa Sheria za nchi,"amesisitiza.
Waziri
Mpina ameagiza wenye meli hizo kuzingatia masharti ya leseni zao
zinazotaka kuwepo na asilimia 10 ya mabaharia wa kitanzania ndani ya
meli zinazoingia kuvua katika Bahari kuu upande wa Tanzania.
Kwa
upande wa Kamishna wa Oparesheni wa Mamlaka ya kudhibiti na kupambana
na Dawa za kulevya, Luteni Kanali Fredrick Milanzi amesema meli hiyo
baada ya kukaguliwa imekutwa na mapezi kilo 90 ya samaki aina ya papa na
bastola yenye risasi 10 ambayo inaendelea kushikiliwa na Ofisi ya Mkuu
wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Mtwara hadi hati za umiliki
zitakapowasilishwa.
Pia
mwenye meli atatakiwa kuhakikisha anawasafirisha mabaharia kurudi nchi
zao kwa madai hawataki kuendelea kufanya kazi kutokana na kukiukwa kwa
mikataba yao ya kazi.Aidha samaki wasioruhusiwa kuvuliwa kwa mujibu wa
leseni ya uvuvi iliyopewa meli hiyo ( Bychatch) watabaki kuwa ni wa
Tanzania na watauzwa kwa mnada na fedha zitakazopatikana kiasi cha sh
milioni 12 zitaingizwa kwenye Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu (DSFA).
Naye
Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bahari Kuu, Hosea Mbilinyi
amesema hatua zinachukuliwa kwa sasa zimelenga kudhibiti uvuvi haramu na
utoroshaji wa samaki na mazao yake nje ya nchi na kwamba operesheni
hizo ni endelevu na hazitambakiza mtu hata mmoja.
Wakati
huohuo, Wakili wa Serikali kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali
Divisheni ya Mashtaka Makao Makuu Dar es Salaam, Wankyo Simon amesema
makosa hayo adhabu yake ni kubwa na wanapaswa kuzingatia muda uliotolewa
na Waziri wa kulipa faini.
Waziri
wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina pamoja na Kaimu Katibu Tawala Wilaya ya
Mtwara Francis Mkuti wakionesha baadhi ya Samaki waliovuliwa na Meli
hiyo.
Hosea
Mbilonyi Kaim Mkurugenz mamlaka ya Usimamiz wa Bahari Kuu DFSA
akimuonesha waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina shehena ya Samaki
tani 4.5 wasiotakiwa kuvuliwa ambao wanatakiwa Kupigwa Mnada Siku
Yoyote.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina akilekea katika Meli Buah Naga one kukagua Samaki walivuliwa kinyume na Taratibu.
Post a Comment