PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: MWANASIASA MAARUFU NCHINI KINGUNGE NGOMBARE MWIRU AMEFARIKI DUNIA ALFAJIRI YA LEO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
...



Taifa la Tanzania limeamshwa na taarifa za kushtusha zilizoenea mitandaoni asubuhi hii ya leo ya February 2, 2018 ya kwamba Mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru amefariki dunia alfajiri ya leo.

Mzee Kingunge alikuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake Jijini Dar es Salaam takriban mwezi mmoja uliopita.

ikumbukwe tu mnamo january 4, 2018 Mke wa Kingunge Peras Ngombale mwiru alifariki dunia kutokana na ugonjwa wa kupooza kipindi ambacho Mzee Kingunge alikuwa tayari anapatiwa matibabu ya majeraha hayo hospitalini. 

Katikati ya mwezi January mtoto wa marehemu, Kinjekitile alisema  kuwa hali ya baba yake ilikuwa ikiendelea kuimarika kasoro miguu ambayo bado ilikuwa ikisumbua.

Tunatoa pole sana kwa familia, ndugu jamaa na marafiki na pia watanzania wote kwa kumpoteza mtu muhimu sana katika mustakabali wa siasa za Tanzania.

Raha ya milele umpe ee Bwana na mwanga wa milele umuangazie apumzike kwa amani Amina.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top