PRINCE MEDIA TZ PRINCE MEDIA TZ Author
Title: VIJANA WAOMBWA KUTUMIA FURSA YA UMEME KUBUNI MIRADI YA MAENDELEO
Author: PRINCE MEDIA TZ
Rating 5 of 5 Des:
    Vijana wasomi na wajasiriamali nchini, wametakiwa kwenda vijijini kubuni miradi midogo midogo ya maendeleo, kutokana na kuimarika...
 Image result for VIJIJI VYENYE UMEME NCHINI TANZANIA
 
Vijana wasomi na wajasiriamali nchini, wametakiwa kwenda vijijini kubuni miradi midogo midogo ya maendeleo, kutokana na kuimarika  upatikanaji  wa nishati ya umeme vijijini na ili waweze kujiletea maendeleo .

Ushauri huu umetolewa jijini Arusha katika mafunzo kwa vijana kutoka maeneo mbalimbali ya nchi mafunzo ambayo yameandaliwa na Taasisi ya  Energe Change Lab   kwa udhamini wa mashirika ya kimataifa ya Hivos na iied , jijini Arusha.

Akitoa mada katika mafunzo hayo, Lilian Madege akisema upatikanaji wa umeme vijijini unapaswa utumike kama fursa kwa vijana   kubuni miradi midogo ambayo hapo awali ilikuwa ni vigumu kutekelezeka kutokana na kutokuwepo  na huduma ya umeme wa uhakika.

Madege alisema Tanzania kwa sasa upatikanaji umeme katika maeneo mengi unaridhisha hivyo, badala umeme huo kutumika majumbani pekee unapaswa kuwa fursa kwa vijana vijijini kuwa na miradi ya maendeleo.

Akizungumza kwenye mafunzo hayo, Filomena Philipo ambaye ni mjasiliamali mdogo alisema kuwa ,  mtandao wa upatikanaji wa nishati ya umeme katika maeneo ya vijijini kumechagiza kwa kiasi kikubwa maendeleo ya vijana lakini bado kuna  changamoto ya ukosefu wa mafunzo kwa vijana ni  kwa jinsi  gani wanaweza kutumia nishati hiyo kwa upana zaidi.

"tunaomba mafunzo zaidi kwa wajasiriamali vijijini ili kuweza kutumia umeme kama moja ya fursa za kiuchumi hivyo mradi kama huu Energ Safari unapaswa kuendelezwa"alisema

Katika mradi huo kwa kutambua fursa zitokanazo na umeme, ambao unafadhiliwa na mashirika ya kimataifa ya  Hivs na iied  vijana walioshiriki walipata fursa ya kutembelea vijiji kadhaa mkoani Arusha na kuona fursa zinazoatikana na pia changamoto ambazo zinazuia umeme kutumika katika miradi midogo kwa vijana.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top