Akikabidhi vifaa hivyo Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Arusha Kamanda Kennedy Komba amesema Jeshi hilo lina wajibu wa kuhakikisha ujenzi wa nyumba za makazi unazingatia vigezo vyote vya usalama, wao kama Jeshi wanaunga mkono jitihada za Rais Magufuli katika kuhakakikisha makazi ya askari polisi yanakua bora.
“Sisi kama Jeshi la Zimamoto na uokoaji tunaunga mkono jitihada za Amiri Jeshi Rais Magufuli sambamba na wadau wengine waliochangia ujenzi katika kuhakikisha nyumba hizi mpya za askari ambazo ziliungua moto miezi michache iliyopita zinakuwa salama kwa kuweka vizima moto katika kila nyumba kama matakwa ya usalama yanavyohitaji.” Kamanda Komba.
Naye RC Gambo amelipongeza sana jeshi hilo kwa kuonyesha moyo wa kujali jitihada za Rais na wao kufanya kitu ambacho kinatuma ujumbe kwa jamii juu ya umuhimu wa kuzingatia usalama dhidi ya Majanga
Ujenzi wa nyumba hizo 31 kwaajili ya makazi ya askari polisi umetokana na janga la moto lililosababisha jumla ya kaya 13 za askari katika kituo kikuu cha Polisi mkoani Arusha kupoteza makazi na mali miezi michache iliyopita.
Mradi huu wa nyumba za polisi umegharimu zaidi ya shilingi milioni 540 ambapo shilijngi milioni 260 zimetolewa na Rais Magufuli.
Post a Comment