Naibu
Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua eneo la uchimbaji
madini ya makaa ya mawe katika kijiji na Kata ya Magamba baada ya
kuwasili kwa ziara ya kikazi kukagua miradi ya uchimbaji madini Mkoani
Songwe, Leo 23 Februari 2018.
Naibu
Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisalimiana na kamati ya
ulinzi na usalama Wilaya ya Mbozi mara baada ya kuwasili kwa ziara ya
kikazi kukagua miradi ya uchimbaji madini Mkoani Songwe, Leo 23 Februari
2018. Picha Zote Na Mathias Canal-Wazo Huru Blog
Naibu
Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua eneo la uchimbaji
madini ya makaa ya mawe katika kijiji na Kata ya Magamba baada ya
kuwasili kwa ziara ya kikazi kukagua miradi ya uchimbaji madini Mkoani
Songwe, Leo 23 Februari 2018.
Na Mathias Canal, Songwe
Naibu
Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko ameagiza wamiliki wa kampuni
za uchimbaji wa Madini kote nchini kuwapatia mikataba ya kazi
wafanyakazi wote pasina kubagua.
Mhe
Biteko ametoa agizo hilo Leo 23 Februari 2018 wakati alipotembelea eneo
la uchimbaji wa makaa ya mawe katika Kijiji na Kata ya Magamba,
Wilayani Mbozi linalomilikiwa na kampuni ya Magamba Coal Mine.
Alisema
amejiridhisha kuwa wafanyakazi wengi katika migodi mbalimbali nchini
ukiwemo wa Magamba hawana mikataba jambo ambalo linafifihisha uhakika wa
ajira zao.
Aidha,
Naibu Waziri huyo wa Madini ametoa siku 14 kuanzia Leo 23 Februari 2018
mpaka 9 Machi 2018 kwa kampuni ya Magamba Coal Mine kuwa wamekamilisha
taarifa ya utekelezaji wa maelekekezo ya ukaguzi wa migodi yaliyotolewa
kwao na Ofisi ya Madini kanda hiyo.
Alisema
kuwa endapo watashindwa kufanya hivyo ni wazi kuwa watakuwa wamekiuka
masharti ya leseni zao na wajibu wao kwa jamii inayowazunguka na hivyo
Wizara itawachukulia hatua bila kuchelewa.
Sambamba
na hayo pia kampuni hiyo imetakiwa kuboresha na kuwa na mahusiano
chanya na kijiji cha Magamba na serikali kwa ujumla ikiwemo kusaidia
kuboresha baadhi ya maeneo ikiwemo sekta ya afya na elimu.
Naibu
Waziri wa Madini akiwa katika ziara ya kikazi katika Mkoa wa Songwe
alisema kuwa serikali imekusudia kurejesha uchumi fungamanishi kwa
wananchi hivyo kampuni haziwezi kuwa na uchumi imara kama zitasalia
kuendesha migodi pasina utaratibu wa kisheria.
Post a Comment