Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Taifa ya Mbolea (TFC), Salum Mkumba (kushoto), akizungumza na viongozi wa Kampuni ya Premium
Agro Chem Limited inayosambaza mbolea alipofanya ziara ya kikazi ya
siku mbili jana na leo jijini Dar es Salaam kujionea zoezi la
kusafirisha mbolea kwenda mikoani. Kutoka kulia ni Meneja Masoko wa
kampuni hiyo, Brijesh Barot, Mkurugenzi Mtendaji, Sagar Shah na
Oparesheni Meneja, Rhoda Mwita.
Wafanyakazi wa kampuni hiyo na Askari
wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), wakipakia mbolea hiyo kwenye
gari tayari kwa safari ya kwenda mikoani.
Malori ya JWTZ yakiwa katika foleni ya kupakia mbolea hiyo.
Shehena ya mbolea hiyo ambayo inasafirishwa kwenda mikoani kwa wakulima
Mbolea ikibebwa kuingizwa kwenye malori tayari kwa safari ya kupelekwa mikoani.
Malori yakiwa katika foleni ya kupakia mbolea hiyo.
Maghara ya kampuni ya Premium Agro Chem Limited yenye mbolea hiyo.
Na Dotto Mwaibale
KUFUATIA agizo la Rais Dkt John Pombe
Magufuli, kwa Wizara ya Kilimo, kuhakikisha ndani ya siku saba kumaliza
malalamiko ya mahitaji ya mbolea kwa mikoa ya Katavi na Rukwa, Kampuni
ya Taifa ya Mbolea (TFC) imeanza mara moja kuteleleza agizo hilo.
Waandishi wa Habari jana na leo
wameshuhudia watendaji wa TFC wakihaha kutafuta magari ya kukodi kwa
ajili ya kusafirisha mbolea kuipeleka mkoani Rukwa na Katavi, ambapo
zaidi ya tani 600 zimeanza kusafirishwa kuanzia juzi siku ya agizo
hilo.
Akizungumzia hatua hiyo, Mkurugenzi Mkuu
wa TFC, Salum Mkumba, alisema mara baada ya taarifa ya Ikulu juzi,
waliamua kuanza kupakia mbolea hiyo, kwa kutumia magari makubwa (malori)
ya kukodi pamoja na magari makubwa ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania
(JWTZ).
“Kwa sasa sisi TFC hatuna akiba ya
mbolea, lakini hawa wenzetu wa Primium Agro Limited, wanayo akiba ya
kutosha, hivyo tunachukua kwao kwa makubaliano maalum,” alisema Mkumba.
Mkumba aliongeza kusema kwamba, kutokana
na uzito wa agizo hilo lililotolewa na Rais Magufuli, wameongeza nguvu
ya magari, yanayoelekezwa mikoa ya Katavi na Rukwa, ambako mahitaji ya
mbolea hiyo ni makubwa kwa sasa.
Alisema nusu saa baada ya tamko la Rais
Magufuli, alipokea taarifa kutoka kwa Waziri wa Viwanda na Uwekezaji
Charles Mwijage, akimtaka kuhakikisha wakulima kwenye maeneo husika
wanatulia kwa kupokea mbolea.
“Mbolea hii inapelekwa kwa wakulima kote
nchini na itauzwa kwa bei elekezi ya szerikali, na ninawashukuru hawa
wenzetu wa kampuni ya Premium Agro Limited kwa kuwa tayari kushirikiana
kwa maslahi ya wananchi na Taifa letu,” alkisema Mkumba.
Mkumba alisema wameamua kuingia
makubaliano na kampuni binafsi ya Premium Agro Chem Limited, kupeleka
mbolea hiyo kwenye maeneo hayo na mengineyo nchini yenye mahitaji,
lakini akiamini kuwepo kwa unafuu kwenye maeneo mengine.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa
kampuni ya Primium Agro Chem Limited, Sargar Shah, alisema kwamba
makubaliano na TFC ni kupakiwa kwa zaidi ya tani 1000 za mbolea hiyo
kwenda katika mikoa ambayo wo hawana mawakala na kurahisha upatikanaji
na pia kwa bei elekezi ya serikali.
Meneja Biashara wa Primium Agro Chem
Limited, ambaye kwa sasa ndiye anayesimamia zoezi hilo Brijesh Barot,
alisema wamejiandaa vizuri kufanya kazi hiyo mchana na usiku kwa nia ya
kufikia malengo ambayo serikali imeyahitaji.
Barot alisema kampuni hiyo tayari
kuanzia mwezi Septemba, imesambaza kwa wakulima kupitia kwa mawakala wao
zaidi ya tani 19,500 za mbolea ya kupandia aina ya Urea, ikiwa kwenye
ujazo wa kilo 25 na kilo 50.
Barot aliongeza kusema kwamba, kampuni
yake imeendelea kusambza na kuuza kwa wakulima mbolea zaidi kwa bei
elekezi, licha ya kuwa tayari walimaliza kuuza tani 3,500 zilizoagizwa
na serikali na kutakiwa kuuzwa kwa bei elekezi.
“Sisi ni watanzania, wafanyabiashara
wazalendo kwa nchi hii, hatutaki kufanyakazi kwa ajili ya kutafuta
faida,badala yake tunaungana na Mheshimiwa Rais Magufuli, kuisaidia
jamii kwa kufanya kazi ” alisema Barot.
Post a Comment