Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akishiriki ujenzi wa
vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Iyera wakati akiwa ziarani
Mkoani Mbeya, Jana 2 Januari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikabidhi mifuko 20 ya
saruji kwa ajili ya kuongeza nguvu katika ujenzi wa vyumba vya madarasa
shule ya Sekondari Iyera wakati akiwa ziarani Mkoani Mbeya, Jana 2
Januari 2018.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akichanganya udongo
wakati akishiriki ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya
Sekondari Iyera wakati akiwa ziarani Mkoani Mbeya, Jana 2 Januari 2018.
Wengine (Kulia) aliyeshika jembe ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe Paul
Ntinika na Kushoto ni Diwani wa Kata ya Iyera (CHADEMA) Mhe Charles
Mkera
Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akipanga mawe kwenye
msingi wa darasa ishara ya mafundi kuanza haraka ujenzi wa vyumba vya
madarasa katika shule ya Sekondari Iyera wakati akiwa ziarani Mkoani
Mbeya, Jana 2 Januari 2018.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akimpongeza Diwani wa
Kata ya Iyera (CHADEMA) Mhe Charles Mkera kwa kushirikiana na serikali
na kuhamasisha wananchi katika ushiriki wa ujenzi wa vyumba vya madarasa
katika shule ya Sekondari Iyera wakati akiwa ziarani Mkoani Mbeya, Jana
2 Januari 2018.
Na Mathias Canal, Mbeya
Maendeleo
ni mchakato wa kujenga jamii endelevu, yenye kujiamini, kujituma na
uwezo wa kushiriki, kwa misingi ya usawa na kuheshimiana, katika kubuni,
kuandaa na kutekeleza mipango ya kujiletea “maendeleo” na kutumia
matokeo ya kazi zao.
Naibu
Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa amekuwa mwalimu mzuri wa
somo la Uraia Mkoani Mbeya akifundisha kuhusu umoja na mshikamano huku
akisisitiza kuwa Maendeleo ni dhana pana kwa wananchi na hayapaswi
kufanywa kwa mipaka ya vyama vya siasa.
Mhe
Mwanjelwa ameyasema hayo Jana 2 Januari 2018 wakati akizungumza na
wananchi na mafundi wanaojenga majengo ya Shule ya Sekondari Iyera ili
kutatua changamoto ya kuwa na vyumba vingi vya madarasa kwa ajili ya
kuhimili wingi wa wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza
mwaka huu.
Amewasisitiza
mafundi hao kujenga madarasa hayo kwa haraka na viwango vya hali ya juu
kwani shule zinatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni huku shule hiyo
ikiwa na upungufu wa vyumba vinne vya madarasa.
Mhe
Mwanjelwa alisema kuwa tangu serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli
kutangaza utoaji elimu bure kuanzia ngazi ya shule ya msingi hadi
sekondari kumekuwa na ongezeko kubwa la wananfunzi wanaojiunga na masomo
ikiwa ni pamoja na kurejea shuleni kwa wananafunzi waliokata tamaa ya
kuendelea na masomo.
Alisifu
juhudi za Uongozi wa Wilaya ya Mbeya kwa kushirikiana kwa pamoja na
wananchi katika shughuli za maendeleo huku akiipongeza Halmashauri ya
Jiji la Mbeya kwa kufanya vyema na hatimaye kuongoza kwa ufaulu wa
wanafunzi dhidi ya Halmashauri zingine za Mkoa wa Mbeya.
Post a Comment